Umeshawahi kuua?

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Hivi inakuwaje hadi mtu anafikia hatua ya kumuua mama yake au/na hata baba yake?

Inakuwaje mtu anafikia kumuua dada, kaka, binamu, shangazi, au mjomba?

Ushawahi kukutana na mtu anayedanganya kuwa mtu wake amekufa au kafa?

Mtu unatega shule halafu unatoa kisingizio cha fulani kwenye familia yenu kafa.

Au unasema mama yako mzazi ni marehemu ilhali ni mzima.

Watu wa hivi tuwaweke kwenye kundi gani?
 
Mi sijawahi, ngoja waliowahi waje watuambie walikuwa wana maana gani
 
Hiyo ipo sana Nyani Ngabu.....kuna watu wala hawaoni hatari kuua wapendwa wao kwasababu ambazo wala hazina maana kabisa......ila pia kuna wengine huwa wanasema nisingeua pale kibarua kingeota nyasi so imenibidi na Mungu anisamehe!


Mie sijawahi bado!
 
Last edited by a moderator:
Hiyo ipo lakini unatakiwa kumuua marehemu na si mtu mzima i mean aliye hai.
 
Niliwahi kuuwa bibi ili kupata ruhusa kazini...lkn alikuwa marehemu wa siku mingi.
 
Nyani Ngabu, hiki kitu hata mimi chanishangaza! Nafikiri huwa wamekosa ufahamu juu ya uzito wa hayo maneno wanayoyatamka na madhara yake!
 
Last edited by a moderator:
Nimewahi kuua tena kwa kuchinja kuku wengi sana!
 
Hii inafanana na kuua demu? Yaani kumega?
Utasikia jamaa anajisifia nimetoka kuua
 
kuna sekta moja ni maarufu kwa kuua tena mchana kweupe.

Ngoja waje.
 
Kuna demu nilimpiga chini......

akanywa sumu na kufa.......
 
mazigira ndio yanachangia kunakuua kwa kutokusujudia au kunakuua kwa kusujudia ndio maana ni coplex kulezea kilichopo hapo au kusema mama,baba,kaka,etc. amekufa ili upate rambi rambi na hii watu wengi wanaifanya sana
 
nimeshasikia watoto wakijifanya yatima ili wapate ada kutoka taasisi au wasamaria wema!! sijui wazazi wao hufikiriaje mpaka kufikia hatua kama hiyo, kwa kweli inasikitisha maana haya ni malezi mabovu sana wanayompa mtoto wao 🙁

nitawaita mafukara wa fikra because I lack of a better term
 
Je wale wanaopiga PURI [masturbation] hawaui? kama ni wauaji basi mie niliua sana nilipokuwa National service!!
 
nusu ya wanawake wasomi tz wanaweza kuwa wameshawai kuua hadi wakachoka....kuchoropoa mimba nako ni kuua kiumbe hai yaani binadamu. Mungu na awasamehe!
 

NN whats the big problem hapa? Imekatazwa wapi specifically kusema flani kafa kumbe hajafa? (Zaidi ya kua ni vibaya kudanganya) si uongo tu kama uongo mwingine?
Au ndio mnaimani kua maneno huuumba?
It's an exaggerated notion! Haina basis yoyote zaidi ya main Principle ya kutokudanganya, otherwise ni primitive taboo!!

Mind you I will never say any member of my close family is dead!! (Contradictory sio!) Just for the fact that by chance it might happen and the guilt might kill me even though I know I had no part at all in the demise!
 
Kwani ndo anakufa kweli bwana.WAULIZENI BODI YA MKOPO(HESLB) WAMEPELEKEWA VYETI VYA VIFO VYA KUFOJI ILI WATU WAPATE BOOM.
 

Wewe unaweza kumwambia mtu kuwa baba na mama yako wote wamekufa wakati ukweli wa mambo ni kwamba hawajafa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…