Umetoa msaada ndiyo hatukatai sasa ni kwanini utangaze?

Umetoa msaada ndiyo hatukatai sasa ni kwanini utangaze?

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
6,944
Reaction score
14,351
Mungu ni mwema nyote.

Wakuu mtakubaliana na mimi kuwa misaada ni mizuri pale inapohitajika hasa unapokuwa na shida
bila shaka ukipata utatuzi wa shida yako utafurahi sana na kumshukuru Mungu.

Changamoto kubwa ni hii ya kutangazwa yaani aliyekupa huo msaada anaanza kujisema tena na
anasema hadi shida yako. Hii huleta fedheha kubwa sana kwako wewe uliyepewa huo msaada.
Jamii itakuona huna maana ndio maana ulisaidiwa.

Mimi tangu nijiunge na ukurasa wa Malisa G facebook Nimeona huyu kijana mwenzetu akisaidia watu wengi sana wenye uhitaji huyu malisa daima huwa namuombea sana aendelee kuwepo zaidi. Nimeshuhudia mara nyingi sana akileta watu wenye uhitaji ili tuwasaidie mwenye chochote kitu hata kama ni Tsh500 wewe tuma tu .

Binafisi mimi nimekuwa ni kiguswa moja kwa moja na huwa nachangia kulingana na uwezo wangu.
Kwa macho yangu nimeona wajane wakijengewa nyumba za kisasa zaidi na kupewa mtaji wa biashara.
kubwa kuliko ni kuwasadia wenye magonjwa makubwa yanayo hitaji hela nyingi ili wafanyiwe matibabu
na kwa hakika huyu kijana tumeona wagonjwa wengi sana wakipona.

Lakini katika misaada yote hiyo anayo ifanikisha sijawahi ona sehemu au mahali popote kwenye nyumba ya mjane kuna bango linalo sema nyumba hii ulijengewa na watu waliojitoa mitandaoni kukusaidia.

sijawahi ona yaani nyumba inajengwa hadi inakamilika pamoja na masofa kabati nk unakadhiwa bila ya kuwa na tangazo lolote.Hii huwa naona ni njema sana na ndo maana halisi ya sadaka {msaada}


Kitu kinacho nikera na kunifikirisha ni hii misaada serikali yetu inapewa kutoka huko ma mbele Au hata mashirika fulani fulani tu.

Mfano shirika linajitolea kuchimba kisima kimoja kabla hata hakijakamilika kuna bango kubwa mno pale
limeandikwa kuwa kisima hiki kimechimbiwa kwa msaada wa shirika fln.

Huku kuna company moja ikijenga shule lazima yawepo mabango mawili makubwa mno na yana waka taa
Usiku kucha huku yakisomeka kuwa hii shule ilijengwa ya msaada na kampuni hii.

Sio shule tu kila kitu kikifanywa lazima kiambatane na mabango lukuki.

Amini na waambia kuwa hawa watu kuandika vile hudhihirisha kabisa kuwa sisi hatuna maana yoyote ndio maana tulisaidiwa. Hata wanapoyaona watoto wetu watuone sisi hatuna maana ndio maana tulisaidiwa.

na moja kwa moja hawa watoto{vizazi vyetu} daima watatuona hatukujiweza toka mwanzo na wao kumbe hawatajiweza vilevile na wataishi kwa msaada.

Cha kujiuliza kwani hawawezi kutupa msaada bila ya kutuandikia mabango au wakajenga tu na kutukabidhi?
unakuta choo cha matundu14 tu na bango kubwa eti kwa msaada wa watu wa marekani wakuu hii ni sawa kweli? kizazi chetu na kijacho kitaiga nini kutoka kwetu?

Imagine wewe umejengewa nyumba na jirani yako halafu aandike bango kuwa hii nyumba hii ulijengewa na jirani yako flani.

Nina imani wewe mwenyewe itakuuma mno maisha yako yote kila unaposoma hilo bango bali na hilo hata mke wako na watoto watakuona huna maana yoyote ndio maana ulisaidiwa na jirani yako. ni fedheha hadi unakufa.

SIPENDI MISAADA YA NAMNA HII HUTAKI ACHA.
 
Kama ulisaidiwa kweli unajali nini? Kinachopaswa kikuumize ni kutangazwa ingali hujawahi hata kuomba msaada kwa huyo mtu na Wala huujui msaada toka kwake kabisa
 
Kama ulisaidiwa kweli unajali nini? Kinachopaswa kikuumize ni kutangazwa ingali hujawahi hata kuomba msaada kwa huyo mtu na Wala huujui msaada toka kwake kabisa
Kubali tuu kutangazwa nani alikwambia uombe!
 
Mfano shirika linajitolea kuchimba kisima kimoja kabla hata hakijakamilika kuna bango kubwa mno pale
limeandikwa kuwa kisima hiki kimechimbiwa kwa msaada wa shirika fln.
Mkuu siku zote "ANAYEMLIPA MPIGA KINANDA, HUYO NDIO ANACHAGUA MZIKI GANI UPIGWE"

Hivyo usimchukie mchezaji, bali uchukie mchezo wenyewe.

Be a Man.
 
Back
Top Bottom