Umeumizwa moyo mara ngapi mapenzini?

Nashukuru kwa ushauri Bishanga, huwezi amini huwa natamani hii hali iondoke kwangu ila imeshindikana, iliniathiri kwa kiwango kikubwa sana ndugu yangu, siku nilipogundua huo usaliti Faham zilinipotea kama dk 15, baada ya kuzinduka vikabaki vilio na majuto ya kumwamini mwanadamu kama mimi. Ila nilichojifunza mpaka sasa ni kwamba sintokaa nimwamini mwanaume yeyote mpaka siku naingia kaburini. Nilipatwa na mkasa wa karne ya sayansi na teknolojia! Sijui kama kuna siku ntasahau kabisa.
 
Nimeumizwa mara 1! Sijasahau mpaka leo huu mwaka wa 3. Nikikumbuka naanza kulia upya kama vile ndo tukio la jana yake. Nimejitahidi kusahau nimeshindwa!

Pole sana dada, saa zingine ukiwaza sana unaweza kuanza kuua jinsia husika..
 
Nimeumizwa mara 1! Sijasahau mpaka leo huu mwaka wa 3. Nikikumbuka naanza kulia upya kama vile ndo tukio la jana yake. Nimejitahidi kusahau nimeshindwa!
Njoo kwangu trust me utasahau kila kitu lol
 
Labda mimi tu.
 
Sijaumiza wala kuumizwa ila nataraji kumuumiza mtu. Lol!
 
Aaaah,i thank God,namuomba sana yasitokee yalopita
 
Ndugu yangu BAK utatofautishaje mapenzi ya 'kweli' na 'yaliyojaa usanii'?

Si rahisi kutofautisha hasa pale penzi linapokuwa changa lakini kadri siku zinavyosonga mbele utaanza kuyaona mambo anayokufanyia mwenzio ambayo hayaonyeshi upendo wa dhati na hata uaminifu na mengi mengineyo yanayohusiana na mapenzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…