Dunia uwanja wa fujo, Dunia tambara bovu, Waswahili walisema.
Kuna muda nafsi inachoka kabisa na harakati au mtindo wa maisha ulionao, unatamani kupiga chini kila kitu na kuanza upya kabisa ukiwa focused. Eneo linalochosha zaidi ni namba ya simu ya muda mrefu inayogeuka kuwa mzigo usiobebeka.
Makundi ya WhatsApp yasiyo na kichwa wala miguu, kuwa na namba za watu ambao hamuwasiliani hata miaka 10, na wakikutafuta ujue unapigwa kirungu.
Umewahi kufikiria kubadili namba ya simu kwa lengo la kujipa muda wa tafakari, kujiboresha wewe na kuboresha mahusiano yako ama kupunguza cycle ya watu ukiwa na matumaini ya kuanza upya kabisa?
Kama upo, naomba uzoefu wako. Hasara zipi ulipata na faida zipi ulipata? Naamini penye wengi hapakosi neno la busara.
Mkawe na wakati mzuri.