Umewahi kuchanganya matumizi ya vitu viwili ulivyoshika mikononi?

Umewahi kuchanganya matumizi ya vitu viwili ulivyoshika mikononi?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Hata sijui kwanini huwa inatokea hivi, naamini kuna wanasayansi nguli watatuelezea.

Binafsi nimepatwa na visa hivi vingi na nikabaki kujishangaa.

Nakunbuka kuna siku nimepewa mayai na jirani, basi chap chap nikaenda kuyakaanga.

Ebwana ee!!! mkono moja nina magamba ya mayai mkono mwengine nina kikombe nilichopasulia mayai, cha ajabu nikaweka magamba ya mayai kwenye flampeni (frying pan) alafu kikombe chenye mayai nikatupia kwenye ndoo ya taka taka, nilitamani nijipige makonzi.

Siku nyingine kuna rafiki yangu alikuwa na kikombe cha chai yamoto mkono moja mkono mwengine ana rimoti, nikamuomba anipe rimoti nibadili chaneli yeye alikuwa bizi na chai, si akanitupia kikombe cha chai, aisee ulizuka ugomvi mkubwa nusu tuzichape kavu, naye akawa anajitetea kachanganya mafaili

TUPE MKASA WAKO!!
 
Unaweza kutafuta mkanda chumba kizima kumbe upo shingoni.
 
Back
Top Bottom