Umewahi kuchomwa Sindano ya Ganzi? Leo ni Siku ya Ganzi Duniani

Umewahi kuchomwa Sindano ya Ganzi? Leo ni Siku ya Ganzi Duniani

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Siku hii inalenga kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa ganzi katika matibabu. Pia kuwawezesha watoa huduma za ganzi Duniani kusherehekea taaluma yao.

Kaulimbiu ya siku hii pia inalenga kuongeza ufahamu kwa Jamii kuhusu umuhimu wa ganzi katika Matibabu ya Saratani. Pia, inalenga kuimarisha Huduma za #Ganzi ili kuongeza ufanisi wa Matibabu ya Saratani

William Thomas Green Morton (1819-1868) aliyekuwa Daktari wa Meno katika Hospitali Kuu ya Massachusetts huko Boston, Marekani, ndiye aliyefanikiwa kutumia Nusu kaputi kwa mara ya Kwanza katika Upasuaji wa Kutoa uvimbe shingoni Oktoba 16, 1846

Tokea jaribio hilo Mamilioni ya Watu kila Mwaka wamefanikiwa kufanyiwa Upasuaji Mkubwa na Mdogo bila kuhisi Maumivu yoyote

Kwa Mujibu wa Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) Taratibu kuu za Upasuaji Milioni 230 Duniani kote zinafanywa kwa kutumia ganzi ya kila Mwaka
 
Back
Top Bottom