Umewahi kufanya biashara ikakushinda? Kwa nini? Tupe story tujifunze

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Kwenye suala la biashara ni kugumu sana jamani, kuna watu wanaanza biashara zinashindikana licha ya jitihada ila ngoma inagoma kwenda mpaka mtu anasema isiwe tabu anaamua kufunga.

Wengine ni kupata hasara kwa kukosa wateja, wengine ni kushindwa kusimamia biashara nk

Wewe nini kilikukwamisha?

Yangu ni hi, Nilifungua kibanda cha chipsi, nililenga eneo ambalo lilikua soko, nimefanya mwezi wa kwanza vizuri na pesa nilikua naiona, ila ghafla soko likahamishwa eneo hilo kwa sababu halia rasmi, lilijengwa eneo lingine na sikua nimepata taarifa mwanzo kuwa soko linahamishwa maana sikua mwenyeji wa eneo.

Baada ya hapo nikawa hata nikaange kisado cha viazi haviishi unarudhisha nyumbani kula wenyewe nikarudish vifaa nyumbani.
 
nadhani hiyo ni kitu ya kawaida sana kwenye biashara gentleman,

na ambao wamefanikiwa ni wale ambao hawakukata tamaa licha ya kushindwa mara kwa mara kulingana na changamoto mbalimbali walizokutana nazo, na kuzibadili kua fursa ya kufanya vizuri zaidi biashara zao πŸ’
 
Ukianguka, inuka jifute vumbi endelea na safari!
Hakuna kitu rahisi......
Hata unaemuona pale juu/amefanikiwa alianzia chini akapambana akafikia hapo
 
Poor finance management, na kukosea kufanya evaluation vizuri. ( napo sema hapo kwenye hela ni papana sana ), kutoa hela kwenye kazi hii na kuiweka huku, unapoiweka unakuta imezama maana umeua kwingine, hela kutoka ovyo ovyo ndani ya ofisi pana mambo mengi, nilikuza biashara yangu hadi kwa mwezi ilikuwa inafika 27 hadi 30 millions, ila ikaja kufa na madeni juu, na boashara yenyewe nikaifungilia mbali kidogo iniue na kunifanya nionekane kama tapeli
 
Biashara ilinishinda kwa sababu nilimuachia mtu afanye mimi natokea kupiga hesabu baada hata ya siku 5. Nilitamani niwe napiga hesabu daily ila muda kipengele. Ukikuta shoti ukiuliza mtu hana majibu anakukodolea macho tu.
 
Aisee
 
Mungu ni mwema wakati wote.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Njoo huku mbuyuni songwe tunalala Leo kesho mnada wa maana .
 
Mimi nilianza ghafla nikaanza kuwachukia wateja sitaki wateja waje kwenye biashara yangu. Uchawi upo 🀣
🀣🀣🀣🀣 Nimecheka kwa nguvu. Ilikuwa biashara gani?
 
Hujaombwa ushauri broo, elewa mada mdau
 
Duuuh pole Sana broo, kwaiy ulishindwa kubalance unachoingiza na unachotoa inshort, asante nimenoti hii
 
Hujaombwa ushauri broo, elewa mada mdau
Kwani wew umeambiwa uelekeze watu cha kueleza,
mbona kiherehere cha kubabaika na comment yangu gentleman?

eleza unachodhani ni maoni au mtazamo wako na itapendeza zaidi πŸ’
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…