Umewahi kuibiwa business idea / wazo la biashara ?

Umewahi kuibiwa business idea / wazo la biashara ?

wastani kwa idadi

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2024
Posts
503
Reaction score
1,432
  • mpo mnapiga story mtu anapita nayo
  • umeenda kuomba mkopo benki wanahitaji kuiona business plan wanapita nayo
  • umeenda kwenye kampuni kuuza wazo wanakuwahi
  • n.k.

Umeumiza kichwa kufanya uchunguzi wa soko, location nzuri ya kutega, machimbo, gharama, wateja, n.k.

Ghafla unastuka kuna mwamba anachofanya ni copy paste na wazo lako, unagundua kuna mahali data zimevuja ila kinachokasirisha zaidi umepigwa kanzu ya kikatili bila ruhusa, mbaa zaidi alieiba anapiga pesa za kutosha
 
Wazo linaibiwaje? Haya mambo yapo Tz tu, wazo ni nothing, wazo linakua na value likishawekezwa na kutoa matokeo vijana, kila mtu ana mawazo milioni kichwani lakini hayana maana yoyote hadi yatoe fweza! So hamna anayeiba wazo la ntu yoyote hata ukaliweka hapa jf watalisoma watu 10 tu na watano watalipa dislike na wengine watasoma nusu au robo ni mmoja tu atalisoma lote ambaye ni wewe tu!
 
  • mpo mnapiga story mtu anapita nayo
  • umeenda kuomba mkopo benki wanahitaji kuiona business plan wanapita nayo
  • umeenda kwenye kampuni kuuza wazo wanakuwahi
  • n.k.

Umeumiza kichwa kufanya uchunguzi wa soko, location nzuri ya kutega, machimbo, gharama, wateja, n.k.

Ghafla unastuka kuna mwamba anachofanya ni copy paste na wazo lako, unagundua kuna mahali data zimevuja ila kinachokasirisha zaidi umepigwa kanzu ya kikatili bila ruhusa, mbaa zaidi alieiba anapiga pesa za kutosha
Wewe muibiwa wazo utakuwa ni mjinga mno kuongea kila kitu unachotaka kukifanya mbele za watu. Hakuna wazo jipya ila upya ni jinsi ya kulifanya. Atakachochukua ni jinsi ulivyotaka ulifanye. Pia upumbavu wako mwingine ni kuchelewa kuanza kufanyia kazi wazo lako. Anza kidogo kidogo pumbavu wewe.
 
biashara ni structure kama umekaa katika design board ukadraft wazo lako vizuri.
hakuna atakayeweza na kufanya copy paste yako. wewe ndio Mbeba maono. wewe ndio mwenye kuona wapi unatoboa na changamoto ziko wapi.
mimi huwa siwazi kuibiwa maono maana kuna point siwezi share na kuelezea yaani kwenye engine room au backbone ya biashara hapa sikuambii. utapata ABC lakini mifumo ya wazo huwezi ielewa vizuri, time ndio huwa inatofautisha Mbeba maono na aliyeiba maono.

note. kama unashare na mtu idea yako kwa lengo la kukuza au kutafuta mtaji. kata copywrite ya kile unachoenda kuanzisha, andaa maandishi ya kisheria yanayompa angalizo la kutotumia wazo lako vinginevyo,
kumbuka mawazo yanaweza fanana lakini mifumo ya kuongoza wazo inatofautiana hapo tiyari ni vitu viwili tofauti
 
Hakuna wazo jipya la biashara sidhani kama umeibiwa
Mawazo mapya yapo na ndio yanawafanya watu kuwa matajiri.

Kina Bill Gates wote walikuja na vitu vipya ndio maana ni matajiri mpaka sasa.

Au unataka kuniambia pia kina Mkwawa walikua wanatumia Microsoft??
 
Yalikua mapya kipindi kile sio sasa
 
Sasa unafikiri leo haiwezi kuwa jana ya baadae.

Akili yako ikifikia mwisho wake usifikiri ni kwa kila mtu.

Bado kuna mambo mengi mno ya kugundua na yataendelea kufanyika kila siku.
Tofautisha invention na business idea
 
Sasa unafikiri leo haiwezi kuwa jana ya baadae.

Akili yako ikifikia mwisho wake usifikiri ni kwa kila mtu.

Bado kuna mambo mengi mno ya kugundua na yataendelea kufanyika kila siku.
Niambie ni wazo la biashara gani ambalo halijawahi kufanyika
 
Biashara ni wewe, wazo likitoka kichwani kwako ni tamu kuliko la kusimuliwa au kucopy. Na hakuna kitu kuibuwa wazo huo ni ubinafsi wa kishamba.
 
Back
Top Bottom