KatetiMQ
JF-Expert Member
- Sep 25, 2022
- 249
- 506
Hii haishii tu kwa wanaume hata kwa upande wa wanawake.Kwanini wanawake wenye tabia nzuri sana huishia mikononi mwa wanaume wasiokuwa na nia njema .
Ujumbe huu utakuletea mwanga kuelewa undani wa tatizo.
Baba ni nguzo ya familia,ikitokea nguzo ya familia siyo baba na mama amelazimika kushika usukani husababisha mtoto awe wa kike au wa kiume kuchanganyikiwa ukubwani kuhusu namna nzuri ya kupata mwenza mzuri.
Mama anaweza kumlea mtoto wa kiume kuwa mvulana tu lakini jukumu la kumbadilisha mvulana kuwa MWANAUME lipo mikononi mwa baba.Ikiwa baba siyo mfano bora kwa mtoto wa kiume itamlazimu mtoto wa kiume kuiga sifa za kiume kutoka kwa mama lakini sifa za kiume (Masculine behavior) halisi zinatakiwa kuonekana kwa baba sio kwa mama.
Mwanaume ambaye anakuwa bila uangalizi wa mwanaume Rijali (Masculine man) ambaye anakuwa kiongozi, mpambanaji, jasiri, shupavu,asiekuwa na woga husababisha mwanaume kukosa sifa kamili za baba ndani ya familia.Mwanaume wa kundi hili anaweza kuwa mpole kupitiliza, mkarimu sana,anasaidia sana Watu katika jamii,anajitoa mhanga kuwafurahisha Watu wengine lakini ndani ya familia yake anakuwa hapati heshima yoyote japokuwa nje ya nyumbani Watu wanamuona ni baba bora.
Vilevile mwanaume mwengine anaweza kugeuka dikteta, mnyanyasaji,anatesa sana mke na watoto kwa sababu hajui namna bora ya kuongoza familia.
Angalia mfano hapa chini Mwanamke amepata mwanaume mstaarabu sana,mpole,mwenye huruma, asiyependa ugomvi na migogoro, mwaminifu, mtulivu,mpenda amani,mwanaume anamhudumia vizuri kwa kila kitu lakini kauli ya Mwanamke.
MWANAMKE: Mwanaume wangu ananipenda sana,ananijali,ananihudumia kwa kila kitu,hajawahi kuninyanyasa hata siku moja lakini simpendi,namfanyia vituko kila siku lakini ananiomba msamaha wakati mwingine nafanya makosa kwa makusudi kabisa kumkomoa lakini ananiomba msamaha, nifanye nini ili nimuache bila kumuumiza.
Majibu ya swali lake haya hapa chini.
SABABU 5 ZENYE KUFANYA WANAWAKE WENGI HAWAVUTIWI KIMAPENZI NA WANAUME WASTAARABU SANA
Je umewahi kujiuliza kwanini wanaume wastaarabu sana, wenye upendo, huruma,kujali, unyenyekevu, kusamehe makosa, wenye kutumia lugha ya ustaarabu,wenye kujitoa mhanga,wenye uwezo wa kumfariji mwanamke, wenye uvumilivu, usikivu, uaminifu huwa wanaishia kupata wanawake wenye tabia za ajabu ajabu,ubabe, ukatili, udikteta, hasira kupita kiasi, huzuni sana, wenye kulalamika sana, wasiokuwa na shukurani,wenye kumfokea, kumtukana, kumgombeza, kumkaripia sana mwanaume mara kwa mara?
Halafu wanaume wenye sifa za ubabe, ukatili, udikteta, udhalilishaji,majibu ya mkato,hawana muda wa kujali hisia za Mwanamke wanapendwa sana mpaka unakuta mwanamke anachukua mkopo na kuhatarisha maisha yake kwa ajili ya mwanaume?
Kujua yote hayo kwa undani soma ujumbe mpaka mwisho.
ZIFUATAZO NI SABABU 5 ZENYE KUFANYA WANAWAKE WENGI HAWAVUTIWI KIMAPENZI NA WANAUME WASTAARABU SANA
Sababu hizo 8 ni kama ifuatavyo
1.WANAUME WASTAARABU SANA HAWANA SIFA ZA UONGOZI NDANI YA FAMILIA
Wanaume wengi wenye sifa za upole, huruma,kujali, kunyenyekea sana, kusamehe makosa haraka, uvumilivu kupita kiasi huwa hawana sifa za uongozi.
Mara nyingi wanakuwa kama bendera hufuata upepo kwa maana anakuwa mwanaume lakini maamuzi yote anayofanya anaogopa kumkasirisha mwanamke.
Anaongea kile ambacho anahisi kitamvutia mwanamke, anajali sana, anatumia muda mwingi sana akiwa karibu na mwanamke,anafikiria sana mapenzi kuliko kitu chochote.
Mara nyingi huwa hawana uwezo wa kufanya maamuzi badala yake maamuzi yote huwa wanataka wafanye yenye kumfurahisha mwanamke moja kwa moja jambo ambalo husababisha mwanamke anapoteza hisia moja kwa moja.
Kwa mfano anaweza kuulizwa "leo tunakula nini" mwanaume anajibu tutakula chochote ukipendacho ghafla Mwanamke huonekana mwenye hasira kwa sababu mwanaume haonekani kujua namna ya kumuongoza mwanamke ndani ya familia.
Hata kwenye malezi ya watoto -wanaume wastaarabu sana huonekana hawataki ugomvi na watoto zao hivyo huondoa mamlaka yao ya kiuongozi ndani ya familia na kumuachia mwanamke moja kwa moja.
2. HUWA WANATABIRIKA
Wanaume wastaarabu sana wanatabirika kwa maana Mwanamke akimuomba mwanaume kitu chochote anapewa papohapo, mwanaume anaogopa kumkasirisha mwanamke hali hiyo husababisha mwanamke anamchoka mwanaume haraka.
Ukweli ni kwamba unapoishi na mtu ambaye mnakubaliana nae kwa kila kitu utachoka kumshirikisha kwenye mambo yako kwa sababu unajua hakuna mawazo mbadala atakupatia.
Zipo nyakati Mwanamke anataka kusikia neno HAPANA kwa maana anaomba pesa anaambiwa "sina pesa" hata kama pesa ipo , vilevile anasema nataka kwenda sehemu XYZ anaambiwa hamna kutoa mguu humu ndani.
Kwa wanawake maneno hayo huwa yanazidisha upendo anajisikia kuwa ndani kuna mwanaume Rijali.
Wanaume wastaarabu sana wanakera sana na wanachosha kwa sababu kuna wakati Mwanamke ndiyo anafanya makosa kwa makusudi ili aone hasira za mwanaume cha ajabu mwanaume ndiyo anaomba msamaha hapo husababisha mwanamke anakuwa na hasira kupita kiasi.
3.WANAOGOPA MAHUSIANO YAO KUVUNJIKA
Wanaume wastaarabu sana huwa wanakera sana na wanachosha kwa sababu wao wanaogopa kutengana na wenza wao matokeo yake wao huparamia wanawake ambao hawapo tayari kujenga nao familia.
Wanawake ambao ni "Wife material" huwa wanatafuta ushauri wa namna ya kujiweka karibu na mwanaume iwe kwa kuongea kwa upole,kupika,kufanya usafi, kujipendekeza kwa mama mkwe,n.k ili mwanaume aonekane kuvutiwa nao lakini kwa wanaume wastaarabu sana wao hawana uwezo wa kumpa Mwanamke nafasi ya kujitutumua ili aonyeshe kwamba yeye ni "Wife material" matokeo yake wao wanaume hutumia fedha,nguvu nyingi sana,kujitoa mhanga, kumfariji Mwanamke mara kwa mara ili waonekane ni "Husband material" hili ni kosa kubwa sana.
Kwa mfano mwanamke anaweza kumjaribu mwanaume kwa kutishia waachane lakini hana ujasiri huo cha ajabu mwanaume huanza kulia, kuomba msamaha,kupiga magoti matokeo yake mwanamke anapoteza hisia moja kwa moja.
Wanaume ambao huonekana wenye kuvutia sana huwa kinyume chake.
Wanaume wastaarabu sana mara nyingi huparamia wanawake wenye sifa zifuatazo
I.Mwanamke ambaye amezaa lakini ametelekezwa na mtoto wakati huohuo mwanamke huyo bado anataka kurudiana na baba wa mtoto wake lakini mwanaume mstaarabu sana yeye huanza kumpa ushauri,kukumbusha wema ambao amejitoa mhanga kumfanyia, kumbembeleza sana,kuanza kulia, kutishia kujiua,
ii.Mwanamke mwenye huzuni kupita kiasi ambaye muda wote anahitaji faraja kutoka kwa mwanaume lakini hana cha kumpa mwanaume
III Mwanamke ambaye yupo na tabia za ajabu ajabu wala hana mpango wa kuzaa au kuolewa au kujenga familia halafu mwanaume mstaarabu sana huanza kutumia fedha nyingi sana,kumpa ushauri, kumbembeleza sana ili wajenge familia pamoja lakini huishia kuumizwa na kuachwa.
iv.Mwanamke ambaye amelelewa bila kumuona baba au hana maelewano mazuri na baba yake mzazi,au familia ambayo ametokea mwenye kauli ya mwisho ni mama - hapa mwanaume mstaarabu sana huanza kutumia fedha nyingi sana,kumpa ushauri, kumbembeleza sana ili wajenge familia.Hili ni kosa kubwa sana
Ukweli ni kwamba zipo nyakati mwanamke anataka muachane haitaji risala,haitaji ushauri,haitaji vitisho, haitaji kubembelezwa bali anataka muachane tu aondoke zake hapo wanaume wastaarabu sana huwa wanafeli.
4.WANAOGOPA MIGOGORO
Mwanamke anaweza kupima hasira ya mwanaume kwa kumfokea, kumtukana, kumkashifu, kumkaripia, kumjibu vibaya, kumtishia kumuacha,kupuuza simu za mwanaume,kuomba fedha nyingi sana kuliko uwezo wa Mwanaume.
Hapo anafanya makusudi sio bahati mbaya.
Mwanaume mstaarabu sana hufanya makosa makubwa kama kuomba msamaha,kumpa ushauri, kumbembeleza sana,wanaume wastaarabu sana kuna ambao huwa na hisia kali sana (too much emotion) yaani anakuwa na wivu kupita kiasi na hasira kupita kiasi pale ambapo mwanaume anakuwa haeleweki msimamo
Kosa lingine wanafanya wanaume wastaarabu sana hufanya ni kuuliza "upo na mpango gani na mimi" yaani swali ambalo mwanamke anatakiwa kuuliza unakuta anauliza mwanaume .
5.HAWANA CHANGAMOTO YOYOTE
Kosa lingine wanaume wastaarabu sana ni kwamba wao wanaamini kwamba kwa sababu wao wapo na sifa za upole, huruma, kujali, kunyenyekea, kusamehe makosa, uvumilivu,kujitoa mhanga,kufariji wao wanaamini hiyo ndiyo guarantee ya kupata Mwanamke mstaarabu lakini inakuwa kinyume chake.
Kwa kawaida Mwanamke huwa anapenda afanye juhudi kubwa kuhakikisha anampata mwanaume sio mwanaume kutumia nguvu nyingi sana ili ampate mwanamke.
Angalia "bad boy" huwa hawana muda wa kumfuatilia mwanamke mmoja muda mrefu hali hiyo husababisha kuonekana wenye kuvutia sana kuliko wanaume wastaarabu sana ambao hutumia fedha nyingi sana,nguvu nyingi sana,juhudi kubwa sana kwa ajili ya kumvutia Mwanamke mmoja.
Na mara nyingi wanawake huogopa kuachwa mpweke na wanapoona mwanaume haonyeshi ushirikiano wowote huanza kupiga simu mfululizo,kutuma sms mfululizo,kuomba msamaha hata kwa makosa ambayo hawajafanya hii ni kwa sababu mwanaume haonekani kutumia nguvu nyingi sana kujiweka karibu naye ndiyo maana wanawake wenye kuringa sana hupata wanaume wastaarabu sana kwa sababu wao huwa wagumu kukata tamaa.
Wanawake wengi huamini wanaume siyo waaminifu hivyo mwanaume mstaarabu sana huonekana tofauti na imani ya Mwanamke hivyo husababisha ile hali ya kutaka kumchunguza mwanaume kukosekana hivyo mvuto wa mwanaume unapotea.
MAMBO YA KUZINGATIA
1. Mwanaume anatakiwa kujenga uwezo wa kiakili na kihisia wa kukabiliana na migogoro ndani ya familia
2. Aepuke kuonekana mwenye wivu kwa sababu huo utakuwa udhaifu wake mara kwa mara
3. Kuboresha lugha ya mawasiliano - mwanaume zungumza kwa lugha fasaha ,kwa heshima bila kupindisha pindisha maneno
4. Kuweka mipaka -Kutambua tabia gani mwanaume hawezi kuvumilia kisha kufanya maamuzi magumu pale ambapo HESHIMA imevunjwa ndani ya familia
5. Kila sifa nzuri iwe na kiasi aepuke huruma kupita kiasi, unyenyekevu sana, uvumilivu kupita kiasi, kusamehe kila kosa,aepuke kujali sana,aepuke kutumia fedha nyingi sana ili kujali mahusiano yake na mwenza wake