Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Virusi ni programu ambazo zimetengenezwa kwa ajili ya kuharibu programu nyingine zinazokuwepo kwenye mfumo wa utendaji wa kompyuta au simu.
Virusi vya kompyuta vinaweza kufuta, au kuharibu mafaili, kuathiri mfumo wa utendaji wa kompyuta na kuifanya kuwa nzito kwa kuenea haraka na kushambulia mafaili mbalimbali.
Unahisi Kifaa Chako Kimeathiriwa na VIRUSI?
Viashiria vya kuwepo kwa Virusi katika kifaa chako
•Kupata joto kali unapokitumia
•Programu kuwa nzito kufanya kazi, kujifunga au kujifuta
•Matumizi ya 'Data' kuwa makubwa
Jinsi Kifaa Chako kinavyoweza kupata "Virus"
1. Kubonyeza "Link" au viambatanisho kutoka vyanzo usivyovifahamu
2. Kubonyeza matangango unayokutana nayo kwenye kurasa za Mitandaoni
3.Kupakua "Application" kutoka vyanzo visivyokuwa na Uhakika
4. Kuunganisha kifaa chako kwenye Mtandao wa Intaneti kama vile (WiFi) za umma
Jinsi ya Kulinda Kifaa chako kisipate "Virus"
1. Pakua program za kuthibiti "Virus"
2. Epuka kupakua "Program" usizozifahamu
3. Unda Nywila "Neno la Siri" Imara
Ili kulinda kifaa chako kisipate "virus," ni muhimu kuchukua hatua kadhaa za usalama wa kidijitali. Kwanza, pakua programu za kuthibiti "virus" ambazo zinaaminika na zenye sifa nzuri ili kuhakikisha kifaa chako kinaendelea kuwa salama.
Pili, epuka kupakua programu ambazo hujaziifahamu, kwani zinaweza kuwa na hatari na kuleta madhara kwa kifaa chako.
Mwisho, ni muhimu kuunda nywila imara ili kulinda taarifa zako binafsi na kufikia salama kwenye akaunti zako. Kwa kufuata hatua hizi, unaweza kusaidia kuzuia "virus" na kudumisha usalama wa kifaa chako.