Umewahi kukutana na Madhara gani baada ya kumsajilia mtu laini ya simu?

Umewahi kukutana na Madhara gani baada ya kumsajilia mtu laini ya simu?

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
Kwa mujibu wa Kifungu cha 21 (1) cha Kanuni Za Mawasiliano ya Kielektroniki Na Posta Kuhusu Usajili wa Laini Za Simu mwaka 2025 ni kosa mtu kutumia laini ya simu iliyosajiliwa kwa kitambulisho cha mtu mwingine au kuruhusu laini ya simu iliyosajiliwa kwa kitambulisho chake itumiwe na mtu mwingine

Ukiukwaji wa Kifungu hiki utapelekea adhabu ya kulipa faini isiyopungua Tshs. milioni 3 au kifungo cha muda usipongua miezi sita au vyote

Fahamu Madhara ya Kumsajili Mtu line:

1. Mtu anaweza kutumia laini hiyo kufanya uhalifu, kama utapeli, ulaghai, au shughuli haramu

2. Kwa kuwa laini ya simu itassajiliwa kwenye huduma za Kifedha, mtu anaweza kutumia njia hiyo kufanya miamala isiyo halali na kutakatisha fedha

3. Aliyesajili laini kwa jina lako anaweza kufanya mawasiliano yenye madhara kwa watu wengine na wao wakadhani wewe ndio umefanya hivyo

4. Ikiwa mamlaka zitabaini matumizi mabaya ya laini hiyo, zinaweza kufungia akaunti zako nyingine zote za simu na huduma za kifedha.
 
Back
Top Bottom