Yani unaweza ukajikuta unakosa amani moyoni, ukifikiria ulicho kifanya hukioni!!! Lakini moyo umeinama, huna furaha, yani hujachangamka kwa ujumla.
Lakini ukiangalia umekosea wapi huoni, ukijiuliza sasa kwa nini unakuwa hivi hupatati jibu. Unaweza ukatamani hata kukaa tu mahali peke yako.....hutaki kuongea ongea ingawa wewe ni muongeaji sana. Yani dah unakuwa upo upo tu.......
Hebu nambieni hali kama hii imewahi kukupata, kama ndiyo unafanya nini ili iondoke.
Pole sana LD. Nadhani hii ndiyo inaitwa Depression
Angalia hii link hapa chini labda itakusaidia kujibu maswali yako.
Understanding Depression: Signs, Symptoms, Causes, and Help
Nitakuletea cd ya Mchungaji Mwakasege!
Kwa ufupi ukiona hali hiyo inakutokea, si ya kubahatisha hata kidogo...Ni mzigo wa maombi unakuwa unakukabili, lakini kwa akili za kawaida huwezi elewa..
Kwa habari ya rohoni, upatapo hali kama hiyo maana yake ni amri kuwa kimbia uingie kwa mgoti uanze kuomba haraka sana, maana kuna jambo Mungu anataka kukuonyesha , au kukuonya , au kukuelekeza.
Kama ni msomaji wa bible, Yesu akikaribia kukamatwa na wayahudi aliwaambia wanafunzi wake,,"Nina huzuni kiasi cha kufa"...lakini hakupata kueleza ni huzuni ya namna gani...Lakini pia bible inaeleza juu ya 'kuugua rohoni isivyomithilika"..
Ni hali inayoweza kumpata mtu yeyote, lakini amini usiamini ina sababu zake kwa ulimwengu wa roho!
LD my dear pole kama yamekutokea
Mie yalikuwa yananitokeaga sana
Na tiba yake mi nikawa na chukua gin an tonic
Usema ukweli nilijiingiza kwenye matatizo zaidi..
Naelewa kwamba ni tatizo kubwa sana kumweleza mtu
Lakini kutafuta msaada mapema na kuongea na mtu
unaye mwamini ..
Pole sana dear kama uko kwenye hiyo situation..
LD my dear pole kama yamekutokea
Mie yalikuwa yananitokeaga sana
Na tiba yake mi nikawa na chukua gin an tonic
Usema ukweli nilijiingiza kwenye matatizo zaidi..
Naelewa kwamba ni tatizo kubwa sana kumweleza mtu
Lakini kutafuta msaada mapema na kuongea na mtu
unaye mwamini ..
Pole sana dear kama uko kwenye hiyo situation..
Yani unaweza ukajikuta unakosa amani moyoni, ukifikiria ulicho kifanya hukioni!!! Lakini moyo umeinama, huna furaha, yani hujachangamka kwa ujumla.
Lakini ukiangalia umekosea wapi huoni, ukijiuliza sasa kwa nini unakuwa hivi hupatati jibu. Unaweza ukatamani hata kukaa tu mahali peke yako.....hutaki kuongea ongea ingawa wewe ni muongeaji sana. Yani dah unakuwa upo upo tu.......
Hebu nambieni hali kama hii imewahi kukupata, kama ndiyo unafanya nini ili iondoke.
Dah, LD hata mimi huwa inanitokea hiyo hali na sa zingine hadi machozi yananitoka na ikitokea nimekumbuka tukio baya naweza nikalia kabisa.
Mara nyingi hutokea hivyo ninapokuwa mwenyewe kwahiyo nikihisi kupooza pooza natafuta watu wa kuongea nao au hata simu nipige ilimradi nisihisi upweke.
Pole sana LD hiyo hali ilishawahi nitokea na mimi kipindi fulani nimuuliza mtu mkubwa aliekuwa jirani na mimi akaniambia inatokana na kuwaza sana halafu vitu vyenyewe unavyowaza haujui ufumbuzi wake mfano unawaza kupata pesa lakini hujui utapataje kwa kifupi unawaza vitu ambavyo haviwezekani kwa wakati huo na akaniamia solution ni kwamba ukiona unawaza kitu ambacho unajua huwezi kukipatia muafaka kwa wakati unaotaka kifukuze kabisa moyoni mwako na ndio hapo unatakiwa uingie katika maombi, mimi nilifanya hivyo na nikafanikiwa