Umewahi kukutwa na hili tukio?

Umewahi kukutwa na hili tukio?

Ketoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2015
Posts
1,117
Reaction score
1,966
Kuna jirani yangu ni bachala,hajaoa,ni mtumishi wa umma na amepanga nyumba ambayo ni ya mh hakimu fulani hapa mtaani

Katika hali ya ujana akaingia mahusiano na binti wa Hakimu,huyu binti ni mwanafunzi anasoma shule moja ya bweni,sasa Jana kamuopoa binti kutoka Shuleni kwao muda wa usiku akidhani kuwa alfajiri atamrudisha binti shuleni

Baada ya kumleta binti usiku,kumbe binti ana mapepo(majini) yamemshika na binti kapiga makelele tangu usiku mpaka alfajiri

Alfajiri ndo akawa yamepungua baada ya kuombewa na pasta,ila binti kawa na vidondo mwili mzima,amevimba uso kutokana na kuperekeshwa na hayo madude

Wakati anapiga makelele alijitahidi kufunga mlango ili asitoke nje isije ikawa kesi nzito maana ni mwanafunzi hata hivyo ilishindikana baada ya binti kupata nguvu za ajabu na hatimaye binti akatoka nje akajigalagaza hapo chini karibia saa moja,wakaja wakamtambua ni mtoto wa mh Hakimu na baadae wakamleta pasta wakamuombea

Baadae mama yake binti akapata taarifa akaja akamchukua binti amempeleka hospital kutibiwa kutokana na madonda aliyoyapata

Kijana anasema tangu wafahamiane na huyu binti hata mwezi haujaisha na jana ndo ilikuwa mara ya kwanza kukutana hata hivyo ndo walikuwa wapo kwenye maandalizi ya kusex ndo akashtukia binti analegea na kuanguka chini maana maandalizi yao walianza wamesimama

Kijana ameshindwa afanye nini,mama yake binti wala hajagomba na mh Hakimu kasafiri

Nini atafanya ? Ni mtumishi wa umma
 
Kinachosubiriwa siku zote huwa ni chenji ukununua kitu dukani na si vinginevyo
 
Back
Top Bottom