Umewahi kulazimika kutoa rushwa ili upate huduma fulani?

Umewahi kulazimika kutoa rushwa ili upate huduma fulani?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Wakuu kwema?

images (1) (4).jpeg


Kuna sehemu mbalimbali raia huenda kwa ajili ya kupata huduma, changamoto hutokea pale ambapo mtoa huduma anakataa kukupatia huduma fulani au anakuzungusha kukupa huduma hiyo mpaka utoe cha juu/kipoozeo/kifuta jasho/rushwa.

Ukitoa rushwa mambo yanakwenda haraka, hata zile mashine ulizokuwa unaambiwa hazifanyi kazi au mtandao uko chini kila wakati unapotaka huduma zinapata muujiza na kufanya kazi kama mpya!

Imewahi kutokea ukalazimika kutoa rushwa ili upatiwe huduma uliyokuwa unahitaji?
 
Nilitoa rushwa NIDA ili nipate uthibitisho kuwa ni raia wa nchi hii kipindi hicho nina viambatanisho vya kuanzia babu.

Nilitoa rushwa uhamiaji ili nipate passport mbali ya kuwa na kila kithibitisho.

Nilitoa rushwa polisi ili mtu niliemshataki kwa kuniibia akamatwe, kukiwa na uthibitisho wa video na kukiri kwa mtuhumiwa kuwa ni mwizi.

Nilitoa rushwa bank wanipe bank statement ya pesa zangu mwenyewe kwa vile zilipita dk 5 baada ya muda wa kufunga bank.

Nilitoa rushwa hospitali ya serikali ili nipate medical report ya kuthibitisha kuwa ni mgonjwa na nahitaji kwenda kutibiwa nje (kwa pesa yangu mwenyewe) na hii nikiwa na kila viambatanisho vya kitabibu .

Nchi hii kila kitu ni rushwa rushwa rushwa.
 
Nilitoa rushwa NIDA ili nipate uthibitisho kuwa ni raia wa nchi hii kipindi hicho nina viambatanisho vya kuanzia babu.

Nilitoa rushwa uhamiaji ili nipate passport mbali ya kuwa na kila kithibitisho.

Nilitoa rushwa polisi ili mtu niliemshataki kwa kuniibia akamatwe, kukiwa na uthibitisho wa video na kukiri kwa kumtuhumiwa.

Nilitoa rushwa bank wanipe bank statement ya pesa zangu mwenyewe kwa vile zilipita dk 5 baada ya muda wa kufunga bank.

Nilitoa rushwa hospitali ya serikali ili nipate medical report ya kuthibitisha kuwa ni mgonjwa na nahitaji kwenda kutubiwa nje (kwa pesa yangu mwenyewe) na hii nikiwa na kila viambatanisho vya kitabibu .

Nchi hii kila kitu ni rushwa rushwa rushwa.
Inahuzunisha.... kama uhamiaji kipindi fulani hadi niliacha process za kupata passport, unazungushwa na kila kitu uko nacho!
 
Polisi Hawa jamaa ni wapuuzi sana. Ngoja niishie hapa ila niwapuuzi mno
 
Hakuna hata Mmoja ambaye hajawahi kutoa rushwa na yupo Tanzania hii tusidanganyane unless upo Scandinavia countries
 
Ofisi nyingi za umma kuna mazingira yanawekwa yanayokulazimisha kutoa rushwa ili upate huduma, vinginevyo ukishindwa kujiongeza hiyo huduma hupati kabisa au itakuchukua muda kuipata.

Kuna ofisi moja nilienda kupata huduma fulani nikazungushwa sana ikabidi tu nisepe, wakati natoka nje ya geti mlinzi akanisimamisha na kunipa maelekezo fulani na kunitajia kiwango kinachohitajika ili niweze kufanikisha huduma niliyohitaji.

Nilichogundua ni kuwa unazungushwa ndani, ukiwa unaondoka mlinzi anatumiwa maelekezo ili kukushawishi kuwa huduma unayotaka inawezekana endapo utafanya moja mbili...

Wale walinzi kwenye ofisi za umma wanashirikishwa dili nyingi za rushwa, mamlaka zinazohusika ziwaangalia kwa umakini zaidi.
 
  1. Naam, niliwapa Tanesco kufunga umeme
  2. Masoko ya Serikali kupata eneo ndani ya jengo
  3. City, taa ya gari niliyoiegesha ilining'inia, kusimama kuiweka sawa haooo.. Sio watu
  4. Hospitali za Serikali
  5. Halafu kuna haya madude mawili, yanaitwa polisi na mahakama. Bila rushwa hutoboi na jambo lako..
 
Back
Top Bottom