Umewahi kulipwa deni ulilolipotezea bila kutarajia?

Umewahi kulipwa deni ulilolipotezea bila kutarajia?

LA7

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
655
Reaction score
2,369
Nakumbuka jumapili moja nikiwa Sina hata 100 mfukoni nikiwa nawaza nafikaje kesho chuo maana kwenda na kurudi ni 1200 basi mida ya saa mbili najiandaa kwenda kanisani mara nikapigiwa simu na namba ngeni.

Nikasikia sauti ya mwanaume akiniambia nimsamehe kwani alikuwa amepata dharura hivyo akiniambia nimtumie namba anitumie hela nilokuwa namdai.

Basi sikutaka kujua ni nani nikamtumia namba akanitumia 30,000 baadae nilikuja kujua ni mtu ambaye nilimkopesha mafuta ya alizeti miezi minne iliyopita mpaka nilipoacha kazi ya duka hivo yy alifikiri Bado nipo dukani.

Nilifurahi mno.
 
Huwa inatokea tena pesa yake Huwa inakuja wakati ambao umechalala haswa.
 
Back
Top Bottom