Umewahi kupanda Daladala ambayo konda na Dereva hawaelewani?

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,455
Reaction score
5,134
Ni mara kadhaa nimewahi panda gari konda na dereva wakawa wamepishana kauli hawaelewani wanagombana, ila hii ya leo walizidi.

Leo nimepanda daladala kutoka Tegeta kwenda Mwenge, konda na Dereva wakawa wanagombana, ugomvi wao ulianza kabla sijaingia hivyo sijui chanzo hasa cha kupisha kwao.

Walikuwa wanajibizana na konda akishusha abiria dereva anaondoa gari bila kusubiri ishara ya konda, dereva aliondoa gari na kumuacha, konda katumia bodaboda kukimbiza daladala baada ya kuachwa na gari.

Sasa tumefika maeneo ya Tangi bovu konda akafanya comeback. Daladala ilisimama kama kawaida, dereva akaamua kushuka kwenda kuita watu maana alikuwa analaumu ana konda mzembe, konda akaingia kwenye daladala na kuanza kuendesha, watu walipiga kelele utatuua ila ndio goma limetembea mpaka dereva alipokuja naye kwa boda ndio konda kusimama kumpisha kituo kinachofuaa.
 
Raha za bongo
 
Konda anagonga gari kuashilia Kuna abiria kamuona,dereva anakausha huoni hakuna kituo kwanza we hujui sheria!
 
Hapo inategemea nani kapewa gari na kama wote wameletwa na boss! Yaani huo mtanange sio wa nchi hii.. Hasa "boss" akiwa konda😂
 
Chai
 
Ukiona hivyo jua gari amekabidhiwa konda.

Sasa kakutana na dereva tembo
 
Kuna Moja nilipanda inaonekana walitoka garage Sasa konda akasahau kumwambia fundi aweke bulb na dereva alilipa aisee safari nzima suka anawaka tu huku na kule konda akajitete nilisahau bro dereva akamwambia mbona ulivyo balehe hukusahau kulenga tobo la dem wako???
Aisee tulicheka daladala nzima😁
 
 
Nimecheka ka mwehu,konda itakua mmiliki wa daladala mjomba wake😁😂😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…