JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Wakati nyakati za Uchaguzi zinapokaribia ukiwemo wa Serikali za Mitaa 2024, ni rahisi kwa Mwananchi asiye na Taarifa Sahihi kufanya maamuzi yasiyo sahihi wakati akijiandaa na Michakato hiyo hadi Kupiga Kura.
Maamuzi yoyote Sahihi kwa Mpiga Kura huchangiwa zaidi na Taarifa Sahihi alizonazo kabla na wakati wa Kupiga Kura kwasababu taarifa hizo ndizo humwongoza katika kuamua kumchagua Kiongozi anayemtaka.
Ungana nasi Sept. 30, 2024 Saa 12:00 Jioni ambapo JamiiForums kupitia JamiiCheck kwa kushirikiana na NuktaAfrica itaendesha Mjadala utakaoangazia namna Taarifa Potoshi zinavyoathiri Maamuzi ya Mwananchi katika Kupiga Kura.
Kushiriki mjadala huu kupitia XSPaces ya JamiiForums bofya x.com
-----UPDATES------
INNOCENT MANGU (JamiiCheck)
JamiiCheck ni nyenzo iliyoanzishwa Miaka miwili iliyopita kutoka ndani ya JamiiForums ambayo inatumika kuhakiki taarifa, mada na habari mbalimbali
Jukwaa hili la JamiiCheck.com ni la kipeke hapa Nchini na pengine Duniani kwa kuwa linatumia mfumo ambao hautumiwi na Taasisi nyingi. JamiiCheck.com inaruhusu Wananchi kuhakiki taarifa, kazi hii inafanyika kwa kushirikiana na Wananchi kwa maana wao wanakuwa sehemu ya mchakato wa kuhakiki taarifa
JamiiCheck imekuwa na Program ya kuwajengea uwezo Wadau wengine wakiwemo Waandishi wa Habari ili kuwa katika ukurasa mmoja kwa kuwa suala la uhakiki wa taarifa unahitaji ushirikiano wetu pamoja
Suala lingine ni kuwa, wakati huu ambapo tunaelekea katika Chaguzi, moja ya changamoto ambazo zinaweza kuleta mkanganyiko ni taarifa potoshi, hivyo JamiiCheck inajiandaa katika kuwawezesha Wananchi kupata taarifa sahihi, kwa wakati sahihi ili ziwasaidie katika kufanya maamuzi wakati wa kupiga kura
SAMMY AWAMI (Mwanahabari):
Taarifa potofu zipo za aina mbili, zipo ambazo Mtu au Watu wanaziandaa na kuzisambaza makusudi akijua anapotosha na zipo ambazo zinasambazwa na mtu kwa kutojuaKuna taarifa ambazo zinaweza kuwa ngumu kutofautisha yupi anataka kupotosha na yupi amefanya kimakosa
Mwaka 2019 wakati wa kipindi cha Uchaguzi wa Serikali za Mtaa, nikiwa na wenzangu mitaa ya karibu na Hospitali ya Mwananyamala kuna Wananchi walipoona tuna vifaa wakatupeleka kwenye Shule ambayo walidai ilikuwa ni Kituo cha Kupiga Kura lakini kuna hujuma kutoka kwa Serikalini kwa kuwa ni eneo la WapinzaniBaada ya kuona hivyo, tukarusha kipindi ‘live’ kupitia BBC, wakati kipindi kinaisha TAMISEMI wakapiga simu na kusema tumepotosha kwa kuwa hicho sio kituo, hivyo bila kukusudia tulipotosha kwa kuwa hatukuwa na taarifa sahihi kuhusu kituo hicho kuhamishwa, kwa hali hiyo unaweza kutengeneza taharuki kama hauna taarifa sahihi
Ni muhimu kuwa na taarifa sahihi hasa wakati huu wa Uchaguzi kwa kuwa mambo mengi huwa yanabadilishwa mara kwa maraMfano hata hivi karibuni ndani ya Siku 10 – 12 zilizopita kumekuwa na taarifa nyingi za kupotosha na kama hakuna umakini unaweza kutengeneza tatizo lingine kutokana na kukosekana kwa taarifa sahihi
MPOKI THOMSON (Mhariri Mtendaji MCL/The Citizen)
Wakati wa Chaguzi kunakuwa na “interest” tofauti kutoka kwa makundi ya Wadau mbalimbali, pia kunakuwa na taarifa nyingi potoshi
Sisi (Mwananchi) moja ya jambo ambalo tunalifanya wakati huu wa Chaguzi ni kuongeza umakini zaidi kwenye suala la uhakiki wa taarifa, kwani taarifa inaweza kusambaa kwa kasi kubwaNi kawaida huwa kipindi kama hiki tunatoa angalizo kwa Waandishi wetu, Wahariri na wote wanaohusika na masuala ya taarifa za Chaguzi
Wakati wa Chaguzi ni muhimu kwa chombo chochote cha Habari kuwa makini zaidi ya inavyokuwa siku zote, ndio maana kipindi kama hicho ni kawaida kuona kuna ushiriki wa Wahariri na Waandishi wenye uzoefu na masuala ya chaguzi
Ni muhimu sana kwa Vyombo vya Habari kujipanga mapema kujua nini kinatakiwa kuchapishwa, pia ni muhimu kuwa na ‘factchecking tools’Kuna vyanzo mbalimbali vya kuhakiki habari na ninasisitiza kwa Wanahabari ni muhimu kulizingatia hilo, pia ikiwezekana kutengeneza timu ambayo inaweza kutumika katika zoezi la kuhakiki Habari
Tunajua Vyombo vya Habari Nchini vipo ‘limited’, hivyo kutengeneza FactChecking tool kama ilivyofanya JamiiForums inaweza isiwe rahisi kwa Vyombo vyote vya Habari lakini inawezekana kukawa na dawati lenye Wanahabari Wabobezi kwaajili ya kusaidia
Kuna umuhimu wa kuwa na dawati au Watu wanaoshughulikia masuala ya takwimu, kwani pamoja na yote kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa takwimu katika nyakati za Uchaguzi Suala la kujua idadi ya Watu wangapi wamepiga kura na wangapi hawajapiga nalo ni la muhimu, namba hiyo inaweza kusaidia kutambua uhalisia unaoendelea
INNOCENT MANGU (JamiiCheck)
Kuna Watu ambao kwasasa wameanza kuwa makini kwa kuwa wanajua wakisema taarifa ambazo ni potoshi basi JamiiCheck itawahakiki kama ambavyo imekuwa ikifanya, hivyo hiyo imewafanya wawe makini zaidiPia, tumekuwa tukipitia Sera na Ilani za vyama mbalimbali ili wanapotoa kauli iwe rahisi kuujulisha Umma kuwa taarifa fulani sio sahihi
Ukipita kwenye Jukwaa la JamiiCheck.com utaona tumebaini baadhi ya Akaunti za Mtandaoni ambazo zimekuwa zikihusika kutoa taarifa potofu mara kwa mara, inavyoonekana Wahusika wamekuwa wakifanya hivyo kimkakati kwa kuwa wanapoweka taarifa zao ni rahisi kuona zikisambaa
DANIEL MWINGIRA (Mkufunzi wa Masuala ya Uhakiki wa Taarifa - Nukta Africa)
Dunia nzima inapambana na taarifa potoshi, mfano mwaka huu 2024 kuna Nchi takribani 64 zina uchaguzi, hivyo taarifa potoshi zimekuwa nyingi na zitaendelea kuwa nyingi
'Tools' za kugundua taarifa potoshi zipo za aina mbalimbali, mfano ipo ya kutambua picha au video. Maswali ya kujiuliza ya muhimu ni je picha imetumwa au kupostiwa na nani na katika muda gani?Kuna ‘tools’ za Mtandaoni mfano unaweza kutumia Google ili kutambua picha au video husika, tunachosisitiza ni kuwa kabla ya kusambaza picha au video unatakiwa kujiuliza kwa undani kuhusu hicho unachotaka kukisambaza
Moja ya changamoto kubwa kuhusu taarifa ni matumizi ya teknolojia kubwa, mfano, kuna matumizi ya Akili Mnemba (AI). Kwasasa watu wanweza kutengeneza hadi sauti ya mtu Fulani ili tu waitumie katika kutimiza lengo la kupotosha taarifa
SAMMY AWAMI (Mwanahabari)
Matumizi ya Teknolojia yamefanya kuwe na kazi kubwa katika kutambua Habari Hotoshi kutokana na uwepo wa mitandao mingiNimefurahishwa na wanachokifanya JamiiCheck badala ya kusubiri mpaka mamlaka husika ije itoe taarifa sahihi, JamiiCheck inakuwa mstari wa mbele kutafuta taarifa sahihi, ni muhimu Wadau wote tushirikiane katika kutoa Taarifa Sahihi
Unapoona taarifa ina mashaka ni vizuri kuihakiki kwanza kabla ya kuisambaza, ni jambo la msingi la kufanya ambalo linaweza kukusaidia kupata taarifa sahihi
MPOKI THOMSON (Mhariri Mtendaji MCL/The Citizen)
Wakati wa Uchaguzi mtu anaweza kutoa taarifa ya kupotosha Umma, sio kwasababu ya kupotosha lakini kwa kuwa hana uelewa wa kutosha. Nini kifanyike? Serikali inapofanya kazi na Wadau wa Habari kama vile Vyombo vya Habari inaweza kusaidia kufikisha ujumbe wa elimu kuhusu utambuzi wa Taarifa Potoshi
Kuna umuhimu wa Vyombo vya Habari kuwa na ushirikiano ili kuwa na mfumo au utaratibu wa utoaji wa taarifa sahihi kwa kuwa kukosekana kwa taarifa sahihi wakati wa uchanguzi kunaweza kumfanya Mwananchi kutofanya maamuzi sahihi wakati wa kupiga kura
SAMMY AWAMI (Mwanahabari)
Kunapokuwa na taarifa nyingi potoshi zinaweza kuchangia kutofanyika kwa maamuzi sahihi wakati wa kupiga kura. Pia, zinaweza kuchangia kuongezeka kwa chuki na mwisho wake kukawa na matokeo hasi, ni vitu ambavyo vinatakiwa kudhibitiwa
Kuhusu Waandishi kuwa wanafanya kazi upande mmoja ni maoni ya Wadau lakini nafahamu kuna Waandishi wengi wanafanya kazi nzuri. Inawezekana hakuna ukamilifu kwa asilimia 100 lakini yanapopatikana maoni kama hayo yanawakumbusha
Mbinu za upotoshaji zinaongezeka kadiri siku zinavyosonga mbele, hivyo kuna uhitaji wa kuendelea kutoa elimu kila siku kulingana na taarifa potofu zinavyoendelea kusambaa na kutengenezwa