Umewahi kusoma kitabu, The Richest Man In Babylon? Ulijifunza nini? Kinasaidia?

Nimejiwekea lengo la kusoma kitabu kimoja kila mwezi, nimeshamaliza THINK AND GROW RICH kwenye timetable kinachofuata ni hiki THE RICHEST MAN IN BABYLON.

Shukrani sana kwa kushare kitabu hiki.
Usisahau kukisoma Retire Young Retire Rich cha Robert Kiyosaki huyu mwamba ametema madini humu ukikisoma unaaga umaskini haki
 
Nimejiwekea lengo la kusoma kitabu kimoja kila mwezi, nimeshamaliza THINK AND GROW RICH kwenye timetable kinachofuata ni hiki THE RICHEST MAN IN BABYLON.

Shukrani sana kwa kushare kitabu hiki.
kimekusaidia nini?
 
Msamaria mmoja ajitokeze kutoa summary fupi ya kitabu hiki...isiyo zidi paragraph mbili please
 
kimekusaidia nini?
THINK AND GROW RICH by Napolean Hill, kitabu hiki kimenisaidia sana katika kuhakikisha naendelea kusonga mbele kwa Jambo ninalolifanya yaan kutokukata tamaa.

Pia kimenisaidia kuwa na jicho la tatu la kuona mambo mbalimbali, hususani katika kusimamia ndoto na malengo niliyojiwekea bila kuyumbishwa na maneno au mitazamo ya watu wengine kirahisi.
 
Look here! Ukipata kipato chochote huwe mshahara, mishemishe, nk., mwisho wake hiyo hela unaitumiaje? Kulipa kodi ya nyumba, bills mbalimbali kama vocha, umeme, maji nk. Nauli, michango mbalimbali kama harusi nk. Unapelekea wafanyabiashara wa vyakula, mboga, nguo, vinywaji nk. Mwisho wa siku hela yoote uliyoipata kwa tabu inaisha kanakwamba unafanyakazi ili ukilipwa uigawe hiyo hela na kuwapelekea wengine!! Kwanini hujifikirii wewe ukajilipa angalau 10%. Kumbuka: kama jinsi ambavyo ukishatoa hela kwa ajili ya matumizi niliyoyataja na mengineyo hiyo ndo imetoka sio yako tena na huwezi kwenda kuidai. Ndo hivyohivyo hiyo 10% uliyojilipa siyo yako tena! Usiiguse! Umejilipa! Iache iongezeke hadi muda uliojiwekea ufike na ufungue biashara au iwekeze katika uwekezaji utakaokupa faida. Yahani hiyo hela ianze kukutumikia na kukuletea hela zaidi tofauti na mwanzo ambapo pesa ilikuwa inakutumikisha. Hii ndio siri ya utajiri! Nasisitiza: hiyo 10% siyo yako! Ukiitumia umekwiba! Kwa wakristo inaitwa sadaka (zaka).
 
Napingana na ww mkuu hapo mwisho. Asilimia kumi sio hiyo wanayoiita wakristo.
Ni hivi : ukishatoa 10% yako basi inayobakia ya kuwalipa wengine yaani mahitaji basi unatoa 10% tena ya iliyobakia ndio unatoa kanisani km sadaka au msikitini. So tuseme unakata 20%.
Kumi yako kumi kwa Mungu.

Mfano kipato 10,000/=
10% yako ni 1,000/=
Hapo inabakia elfu tisa
10% ya elfu tisa ni sh. 900/=
Hii 900/= peleka kwa Mungu

Inayobakia ndio matumizi mengine mf kwa mangi, luku ada nk.

Am ready to be corrected.
 
Dah kitabu ni kizuri sana
 
Pointi yangu ni kuweka msisitizo wa kiasi unachoamua kujilipa ili usishbwishike kukitumia. Kama umetenga 10% au 15% kama cummulative income (umejilipa) kwa kipindi kama mtaji, basi imetoka! Usishawishike kuitumia sio yako tena. 'ukifell kuwa na discipline ya kusave! Then forget maudhuhi ya hiki kitabu na utakuwa masikini mpaka kesho. Maudhuhi ya hiki kitabu imejengwa katika 'discipline ya kusave'. KUJIWEKEA AKIBA. Bila kuweka akiba hiki kitabu hakikufai!
 
Hakika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…