UTAPELI UNAANZA WAPI
Kwakua watafuta kazi ni wengi kampuni izi zimeunda mfumo wa kutangaza kazi kupitia njia mbali mbali mfano unaweza kutana na tangazo anahitajika Data clerk officer wanaweka na sifa baada ya apo wanaweka detail za email au namba za simu kwa muongozo zaidi.
Na kwakua watafuta kazi ni wengi wanapita katika site tofauti tofauti watakutana na tangazo wataamua ku apply kwa kutuma CV au kupiga simu kuomba waelekezwe ofisi ziko wapi kupeleka Taarifa zao.
Ukiisha kamilisha Taratibu wao watapitia CV watachukua namba zako na za marefaree na watakupigia simu ufike ofisini siku fulani, baada ya kufika ofisini mtawekwa katika kundi la watu wengi mtaanza pewa detail za kuhusu iyo kampuni na baada ya apo mtaambiwa kujiunga ukikubali utatoa pesa utajaza fomu na lisiti utapewa labda ya EFD au ya kawaida.
Baaada ya kujaza fomu zao utatumiwa msg inayoonesha siku, mahala, saa na kampuni unayotakiwa kwenda kufanya interview.
Kama ukipata kazi mkataba unakuja katika makato ambayo kampuni utakukata asilimia flani mfano 30% katika mshahara wako kwa muda labda wa mwezi 1 au 3.
Mara nyingi interview unazotafutiwa na izi Recruitment Company ni ndogo ndogo ndugu zangu ni kwa wachina yaani wao wanakutafutia kazi kwa wachina ukauze mabegi, saa, vyombo, foodsuppliments, au uzunguke mitaa ya k koo ukipita kila mitaa kuandika taarifa za maduka yana deal na nini na ujira wako ni sh 5000-7000.
Na kama si kwa wachina watakutafutia interview katika vijiwanda vidogo vya masofa, magodoro,au supermarket na sheli.
Sasa kwa mantiki hii jaribu kufikilia unapata kazi mshahara 150,000 toa 30% miezi mitatu na apo ulijaza fomu yao ya 40,000 inamaana watakua wanakukata 45,000 kila mwezi kwa miezi 3 ambapo wewe utabaki na 105,000.
Sasa kwa kiasi hiki cha pesa sawa hauna Ajira ila kwanini uteseke, umesoma kwa shida na gharama kubwa ila ujira wa kazi ni wakinyonyaji sana yani kama unakaa eneo la mbali na kazi hii pesa itakua inaishia kwenye nauli tu.
Ubaya zaidi najua watu wanawajua wachina na wahindi walivyo wanyonyaji na wenye roho mbaya utafanya kazi kama punda na mda mwingine utafanya ata zisizo katika mkataba wako.
Kunautofauti gani wa muhitimu wa chuo na mdada wa kazi za ndani ambae yeye anapata unafuhu kwa kukaa kwa boss, chakula, maladhi na vingine boss anatimiza au muhitimu uyu anatofauti gani na wabeba mizigo au barmaid?
Na izi kampuni ndogo ndogo za kutafuta ajira ndio zinazo haribu taswira ya kampuni kubwa na mda huu wameenda mbali kwakua unatoa CV yako wanachukua namba za marefaree wako wanapigiwa na wanajieleza kana kwamba wanakufahamu sana kwakua detail za CV Wanazo kumconvice mtu ni rahisi sana hivyo kutapeliwa kwa njia hii.
HITIMISHO:
Ukitaka kujiunga na Recruitment agency au Company tafuta zile kubwa kubwa kama Eurolink, Vipaji, Brightermonday especially tafuta zile zinazo operate zaidi ya nchi moja ila nyingi za kwetu wazawa hazina Connection yoyote zaidi ya kuibia wahitimu waliochoka zaidi
Mfano pale Makumbusho stendi kuna kampuni ya Muhindi na mbongo wanajiita JOB JUNCTION hawa jamaa n kampuni ndogo sana hawana website,kijiofisi ni kiframe kimoja, taarifa zao ukitaka wanakwambia njoo ofisini kwetu na ukisearch google hupati taarifa zao kiufupi niwapigaji ndugu yangu aliwai kwenda pale akakuta vijana kama 40 ivi ambao walifanya registration sku iyo yeye akashindwa kwakua alikua hana pesa sasa unapata ona kwa siku moja iyo.
40,000x ada ya kujiunga(20,000) ni sawa na 800,000 per single day kesho yake amerudi tena kakuta wengine inamaana hawa jamaa wanatengeneza pesa ata zaidi ya 10M per months kwakua wahitaji wa huduma ni wengi na kazi watakazo kuunga amini ata wewe unaweza zitafuta kazi za sales zipo nyingi sana.
Lakini pia unapotafuta kazi usipende kutuma CV au taarifa zako katika email ambazo sio za kampuni mfano unapata ujumbe mwalimu wa Chemistry anahitajika Dodoma, Mshahara ni 800,000 tuma detail kwenye email hii.
hatunamajanga@gmail.com unapokutana na tangazo kama ili achana nalo ni matapeli hawa utatuma CV watatumia detail zako kuibia watu kama Refarees wako
Kiashiria cha kampuni kama inatambulika ni
1. Anuani halisi mfano
info@ kazinikwetu.go.tz inamaanisha hii kampuni ina website official ila sio kutuma nyaraka zako katika email ya mtu binafsi inayo kua na gmail, hotmail, yahoo
2. Lazima kampuni iwe na taarifa sahihi mfano unapoingia google lazima utapata location, historia ya kampuni, Mission, vision nk ila kama ukikuta hivi avipo badala yake ni namba za simu anza kushtuka kwanini uitwe ofisini kupata maelezo wanaficha nini awa ndo matapeli wenyewe