Umewahi kutana na tukio lolote lilikouacha na mshangao mkubwa katika soka!!?

Umewahi kutana na tukio lolote lilikouacha na mshangao mkubwa katika soka!!?

carnage21

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2023
Posts
591
Reaction score
1,382
FEBRUARY 14,2018 kwenye mchezo kati ya Real Madrid na PSG lilitokea tukio ambalo lilileta utata sana na wengi wakibakia na mshangao mkubwa huku likihusisha nguvu za giza (Uchawi).

ILIKUWA ni tukio la penati aliyopiga Cristiano Ronaldo 🇵🇹 kwenye ushindi wa Real Madrid wa goli 3-1 dhidi ya PSG kwenye hatua ya 16 Bora ya UEFA. Ronaldo alipiga penalti hiyo ya kimaajabu iliyopewa jina la 'Magical Penalty' na kufunga lakini kabla ya kupiga na kufunga inadaiwa mpira ulinyanyuka juu kabla ya kuguswa na mguu wa kulia wa Ronaldo 🇵🇹.

MPAKA sasa kwenye historia ya Mpira hakuna kumbukumbu zinazoonesha kuwa kuna Mchezaji mwingine ameshawahi kupiga penati ya namna hiyo (Mpira kuonekana unaelea kabla ya kupigwa).

KISA kipi cha Kimpira ambacho kimewahi kukushangaza baada ya kuliona na mpaka leo hauelewi lilitokeaje? 🤔 TUPATIE ushuhuda wako hapa hasa kwa Mpira wa Mtaani (Ndondo Cup) .
 
Unashida ama ya macho yako laa imani ya kishirikina imekujaa.
 
Tukio la Simba kuweza kuwasha moto katikati ya uwanja ugenini tena waki uzunguka kwa imani za kishirikina.

Si tu jambo lile lili huzunisha taifa kwa aibu bali soka la Afrika katika ngazi ya vilabu lilipewa taswira mbaya Katika ulimwengu wa soka.

Pale ndio niliamini walozi hawana mshipa wa aibu kabisa.
 
Back
Top Bottom