Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,931
- 24,816
Kutapeliwa ni kubaya lakini asilimia 90 ya waliotapeliwa walikaribisha mazingira ya kutapeliwa wakiongozwa na tamaa na kutotaka fikiri. Lakini wapo kadhaa ambao waliibiwa Kitapeli kwa kufuata utu au kujali.
Kuna dogo mmoja aliibiwa pikipiki kipindi flani huko nyuma.aliponiambia jambo hili ikabidi nicheke sana hadi machozi kutoka badala ya kukasirika au kumwonea huruma.Ilikua hivi;
Katika mizunguko yake kuna abiria mlemavu wa mguu(alikua kashikilia gongo la kumsaidia kutembea) alimsimamisha, aliposimama jamaa akaomba apelekwe sehemu fulani hivi, dogo hakusita akamsaidia kumpandisha kwenye piki piki haooo safari ikaanza, katikati ya safari yule abiria akadondosha lile gongo na kumwambia dogo limeanguka bahati mbaya.
Dogo akapaki chombo akamsaidia jamaa kushuka na kumuweka chini (maana jamaa alijidai anasikia maumivu sana ya mguu hawezi hata kusimama) kisha dogo akaanza kutembea fasta kurud nyuma kwenda kuliokota lile gongo, ile anainama kuokota kule mlemavu bandia akawasha pikipiki na kuondoka kwa spidi, basi ndugu yangu chombo kikawa kimeenda kwa staili hiyo dogo akabaki na gongo la jamaa kama kifuta machozi anarudi nalo maskani kinyonge.
Kwa hisani ya Mnyenz