Umewahi kutapeliwa baadaye ukaishia kujicheka ulivyo Mjinga ukawapa gwala Matapeli?

Ila wezi bana saa nyingine wanachekesha sana..

Kuna jamaa yangu siku hiyo kaja kijiweni na wezi wake sijui wametoana wapi huko mjini wanataka kumuuzia madini feki. Wamekubaliana waje ofisini jamaa aje awape hela. Wezi wana confidence balaa wanamuambia jamaa "we kama hii biashara umeishindwa jitoe tu kuna jamaa mwingine yuko tayari kutoa hela mida hii..!" Jamaa anang'aka "we una kichaa nini? mi siwezi kujitoa huu mzigo nauchukua" Mpaka kuja kumuelewesha jamaa kwamba anaibiwa ilituchukua muda sana πŸ˜€
 
666 chata,

Hiyo style wamelizwa Sana Washamba pale Posta ya zamani kilipo Kituo Cha Mwendo kasi

Kulikuwa Na Jamaa wanauza Mihogo ya Kukaanga, Juice Na Kachumbari

Sasa Yule anaeuza Kachumbari kaweka Sinia lake la Kachumbari sanjari na Mihogo ya kukaanga lakin Ni Biashara mbili tofauti

Yule Mwenye mihogo hahusiki Na Kachumbari sasa ukinunua Mihogo Ukiona Mwenye Mihogo hakutazami Wewe unajaza mikachumbari kwa FuJo Kumbe wanakuchora tu wanakuhesabia Vijiko ulivyo jaza ukimaliza usogee Pembeni uanze kula wanakustua ulipe pesa yao Na wanakukazia mpaka unalipa

Siku hizi hawapo it was 1980-1990s
 
Hapa ukifikiria utagundua wewe uliacha kufikiri....mjini hapa hamna kitu cha bure. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜… We unapewa juice unakunywa tu ndugu yangu sasa ungekuwa huna pesa si wangeweza hata kukuoa? Epuka hiyo tabia.

666 chata,
 
Jamaa aliona mnataka kumwaribia deal... Mjini hapa. Hakuna deal za kizembe namna hiyo...πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„

 
Aman iwe nanyi wakuu

Huu uzi unatuhusu wale wajanja ambao tulipigwa kiboya sana na wajanja wa mjini tukaachwa kwenye mataa

Aisee iko hivi namna ambavyo nilipigwa kiboya sana

Ilikuwa munamo mwaka 2010 niko darasa la tano mimi beira boy nikiwa nimeagizwa sukari dukan nikaondoka na basikel yangu ya gia ambayo nilikuwa nimeletewa na sister kutoka huko mjini

Nakumbuka ilikuwa mida ya jion ndo nilipopigwa kiboya sana aisee

Nilikutana na jamaa mmoja mshamba mshamba sana jamaa amekaa kama msukuma sijui wa wapi tu yaan

Jamaa akanambia wewe dogo simama, dah bila hiyana si nikasimama aisee jamaa akaanza kunipiga fix kuwa kuna gari limepata ajari na kwenye lile kulikuwa na wazungu wanatoka mgodini geita hivyo wale wazungu walidondosha dhahabu zao hivyo jamaa akaziokota na kwa sasa ni tajiri maana anaenda kuuza mjini

Dah jamaa akaendelea kutiririka namsikiliza tu ndo shetan akanipitia jamaa akanambia nimpe sh elf tano na pia nimpe baskel ile nami anipe madini nami niwe tajiri

Kwa utumbafu pasipo kujua kama naingizwa mkenge si nikampa aisee jamaa akanipa yale madini yaliyo kuwa yakiwaka waka

Akanambia weka mfukon watu wasikuone mdogo wangu hiyo ni bahati yako tu

Daah

Jamaa akachomoka na basikel yangu nikampata sh elf tatu ambayo nilikuwa nimepewa nyumban na MAMA

Nikaanza kurud zangu kwa mguu ile nafika home shap shap nikamfata MAMA ndan nikamwambia mama nimebadilisha baisikel na dhahab, nimepewa dhahabu, mama nani kakupa na hiyo dhahabu iko wapi si ndo nikampa aione

Aisee nilichezea kofi moja machoni had nikaona kama malyenge flan dizain rangi mbili flan hivi

Dah sitakaa nisahau kumbe jamaa alikuwaga amesaga chupa chupa tu wala hazikuwa dhahabu wala nini


Dah nilipigwa kiboya sana aisee


#KIBOYA SANA#


LONDON BOY

Sent using Jamii Forums mobile app
 
siku ya kwanza naingia Ubungo waliniuzia sabuni badala ya simu... wajinga sana wale maboya dadeeki zao, nilinunua nikajiona mjanja nikaweka kwenye begi.. kila nikikumbuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…