Umewahi kutapeliwa mtandaoni au kidogo uingie mkenge? Tuambie ilikuaje uokoe mtu asije kuingizwa mjini (mtandaoni)

Umewahi kutapeliwa mtandaoni au kidogo uingie mkenge? Tuambie ilikuaje uokoe mtu asije kuingizwa mjini (mtandaoni)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Kumekuwa na wimbi la watu kuweka nyuzi kuuliza kama fursa fulani ni kweli au lah, au kama zawadi anayotumiwa ni kweli anapendwa au anataka kuingizwa mjini.

images.png

Tunasikia mara kadhaa watu wanalizwa lakini kenge hawakosi, na mara nyingi huwa inakuwa ni tamaa ya kupata hela ya haraka haraka, na kwa wanaume akishaona mtoto mzuri nyuma mashallah anaingia kichwa kichwa kuja kushtuka kaliwa.

Utapeli huu wa mtandaoni upo kama aina 5 hivi;

1. Wafanyabiashara 'feki'
Hawa wanajifanya ni
wafanyabishara mtandaoni ambao wana maduka kabisa ya mtandaoni na utapeli unatokea pale unapoambiwa utume pesa ili utumiwe bidhaa yako ukiingia ukituma ndio imeenda hiyo. Wengine hutuma lakini unachopokea inaweza kuwa mdoli wa bidhaa halisi yaani mfano unanunua jiko la gesi lakini bidhaa inayokuja ni toi/mdoli wa jiko la gesi😂😂

Hapa Mshana Jr ameeleza kilichomkuta kwenye kupokea bidhaa za matoi badalaa ya kitu halisi - DOKEZO - Utapeli biashara mtandaoni: Shuhuda za watu waliowahi kupigwa na kujuta sana

images (37).jpeg

Na Mkuu hapa ameeleza jinsi ya kuwatambua kwa uzuri kabisa wafnyabishara feki ambao huwa watumi bidhaa ukishawatumia pesa - Viashiria /dalili 6 vya kujua kuwa unatapeliwa mtandaoni

2. Kazi za kuangalia matangazo mtandaoni
Hizi ni kama ponzi scheme scheme tu, ambako unaambiwa utakuwa unaangalia matangazo halafu unalipwa hela, ila ili uanze kuangalia unatakiwa kuweka kiasi cha pesa kwanza na kuna levels. Ili kuwapata watu kirahisi level zinaanzia chini ambayo ni rahisi kumudu, ukishatuma hela imeenda hiyo... mfano wa hii ni LBL ambayo inaenda kwa kasi kutapeli watu. Kwa wenzetu kazi hizi zinafanyika, na ili uzipate mara nyingi inabidi ubadilishe location ya simu yako sababu kwetu Tanzania hatuna mifumo ya kupokea pesa kama paypal. Tapeli wameona fursa na kuweka zao za kupiga watu.

Huyu aliingizwa kwenye scam ya kuangalia matangazo tofauti kidogo na zile ambazo nimekutana nazo so far - Nilivyonusurika kutapeliwa mtandaoni

3. Mahusiano/Urafiki na mtu ambaye anakutumia zawadi hewa na ili upokee unatakiwa kutuma pesa
Hii inafanyika sana kupitia whatsap, facebook, hata insta, ila wa insta na FB utapeli huwa unaenda kukamilika Whatsap.

Hapa huwa unaombwa urafiki kwenye mitandao hiyo na wakati mwingine unashangaa namba imepop tu kwenye whatsapp yako mnaanza chat na mtu. Hii mnaanza kuongea na kuwa marafiki wakubwa wengine huenda mpaka kwenye wapenzi. Mwisho wa siku anakwambia nataka kukutumia zawadi, na inakuwa ni vitu vya gharama kubwa ili kukuingiza mkenge vizuri.

images (36).jpeg

ZInapigwa picha ya hatua zote kuanzia kuchagua, mzingo ukiwa unafungwa kwenye box, ukitumwa kwa ndege na shirika husika linalosafirisha mzigo wako. Mzigo ukifika unatumwa kwenye address ambayo siyo yako. Ambako utaambiwa utume pesa ya usafiri. Kwa jinsi zawadi ilivyo na gharama kubwa hutaona shida kutuma pesa ya usafiri. Ukituma ndio imetoka hiyo.

Kuna mwenzetu anaenda kuwa kenge sasa hivi kama hatasikiliza ushauri wa wadau humu- Ni utapeli au napoteza bahati?

4. Kutumiwa email kuwa ameachiwa urithi na amekuchagua wewe kukuachia pesa maana anakaribia kufa na hana ndugu😂😂😂 the classic!
Hii bana unakutana na email huko wakati mwingine hata rafiki wa facebook. Huko anakwambia yeye ni mtoto pekee na hana ndugu, anaumwa sana na anakaribia kufa ameona akutunuku wewe kwakuwa ni kijana bora sana na unastahili, hivyo mtumie details zako za benki, kijana unatuma fasta wanaenda kwenye acc yako na kukomba hizo af tatu uko nazo.

5. Unaingia mapenzi na mdada mrembo mtanaoni, mnaanza tumiana picha za viungo mwisho wa siku anaanza kuku blackmail ili asivujishe picha zako mtandaoni.
Kwenye hii cases za offline ni nyingi zaidi, ambapo watu wanakuwa wanajuana kabisa uso kwa macho. Unaingia na mtu kwenye mahusiano anaanza kukutumia picha zake za viungo na anakuwa anatuma full body (hasa kwa mtandaoni akitumia picha feki za waingiza ngono mtandaoni na kufanya some edits kidogo), siku anakuomba zako na wewe hata hufikirii mara mbili huyo unatuma, blacmailing inaanza unakuwa kama mgodi wa kutoa pesa.

Najua binti mmoja ambaye amefanyiwa hiki na mtu ambaye walikuwa kwenye mahusiano, mwisho wa siku jamaa akachukua kila kitu cha binti akaboresha biashara yake anapost tu huko insta. Tumemwambia aripoti polisi au alete kesi yake hata hapa JF naamini hata JamiiForums wenyewe wangemsaidia maana wanatetea haki za digitali na kulinda privacy za watu ukizingatia pia sheria ya taarifa binafsi imeshaanza kufanya kazi lakini aligoka kata kata kwa uoga ako nao, yaani na ana ushahidi mpaka wa abuse aliyokuwa anafanyia lakini imeshindikana kutoa case yake nje akiogopa kwa kufanya hivyo picha zitawekwa hadharani.

Njia zipo nyingi sana zinazonyumbulika kutokana na hizo 5, nilizoweka ni baadhi tu nawaachia wadau mje mfunguke nyingine kutokana na experiences zenu.

Kuna wengi humu mshapitia kwenye utapeli wa aina moja au nyingine ama ulitaka kutapeliwa ila ukshatuka, au ukaingizwa mkenge ukaja kushtuka ukiwa umeshachelewa, na wengine ndugu na jamaa wa karibu wameshaingizwa mkenge.

Lengo la uzi huu ni kujuzana ulibamizwa wapi na njia walizotumia ili wengine wajifunze wasijekulizwa.

The flow is yours Wakuu..
 
Niko nasubiria mchongo hapa
 

Attachments

  • Screenshot_20250209-172223.png
    Screenshot_20250209-172223.png
    223.8 KB · Views: 4
Niko nasubiria mchongo hapa
😂 😂 Ukatengenezwe fursa.... umenikumbusha bi mkubwa aliwahi kutafutwa na watu wanakambwa wanataka kuanzisha shamba, sasa anatakiwa atume hela wanunue vifaa kwa kumwagilia sijui, maana mzungu kashindwa kutuma pesa..... nusura wamdake
 
Dah Umenikumbusha kipindi nipo Chuo emails was rocking back then.

Sasa kuna jamaa alipata email ya mdada mrembo yupo kambi ya wakimbizi Sudan sijui wazazi wake wote wamekufa , ana hela nyingi kwenye account...

Mwamba akajua kashatajirika, Muda wote ana furaha 🤣

Kilichompata...
 
Back
Top Bottom