J.K.Rayhope
JF-Expert Member
- Oct 26, 2011
- 316
- 31
Nabaki na maswali mengi sana kichwani,hivi kweli serikali yetu ina mpango gani wa kizalendo wa kukuza utalii wa ndani?Mlima Kilimanjaro uko tz,hivi kweli mjerman anatumia mamilioni ya maili kuja kuuona,halafu mimi mtz nasaga ndala na sina muda wa kufanya utali wa ndani,kwanza mimi kama mtz sijahamasishwa hata na wenye mamlaka,au hata kwa motisha.Kwa ujumla niseme wote tumelala.Kisiwa cha Saa 8 (mfano)akilichopo ndani ya Ziwa Victoria nililazimika kukitembelea baada ya mwl wangu wa somo la history nikiwa Kibasila sec,(Dar) kuzungumzia juu ya kisiwa hicho,nilipotembelea mwanza baadae niliamua kuupata ukweli wa maneno ya mwalimu wangu,niliridhika sana tu,utalii wa ndani kwa tz upo chini sana.Sehemu zote zenye vivutio tuzitembelee tujifunze,au ndio wageni kwanza wenyeji b'dae?Tuwe na desturi ya kujifunza NATUREWORK YA MUNGU.Uone fahari ya kuwa MTANZANIA