Umewahi kuwa na bidhaa zisizouzika ukabaki nazo kwa kushindwa kupata hata mteja wa bei ya hasara?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Nakumbuka 2016 niliwahi kuwa na duka la vifaa vya computer, nikaona nijiongeze ongeze nikaweka mabegi ya laptop kwa mtaji wa milioni 1 nikiamini kwamba yatatoka fasta sana, yaani hayo mabegi yalikuwa hayauziki kabisa, nilitaka niyauze kwa bei ya hasara lakini wapi.

Hadi nafungua duka lingine biashara nyingine hayo mabegi yalibaki nyumbani tu, kazini kuna mtu moja tu ndio alinunua.

Kama zali vile leo ndio nimeyauza japo kwa bei niliyojumulia miaka hio.
 

pole mkuu inatokea mara kadhaa !
Lakini wafanya biashara hawana muda wakuja kukwambia hapa
 
Ndio mambo ya biashara hayo,wenyewe wanasema biashara imani
 
Kwa hiyo leo una 1M mkuu?
Hongera sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…