Umewahi kuwa na rafiki wa kweli ambaye huwezi kumsahau kamwe?

Apumzike kwa amani Joe a.k.a vasco dagama a.k.a chipoli huyu ndie rafiki yangu wa kweli maishani mwangu wakati nipo kwenye harakati za kuisaka shiling nilibuni mradi fulani ila ikawa mtaji hautoshi nilijaribu kusimama kwa ndugu na jamaa ila wakanitosa tu ila nilipomsimulia mwamba akaniambia tulia mzee akauza kipande chake cha ardhi ili anibusti mtaji mwenyewe alikuwa na kauli yake utasikia mzee ukitoboa na mimi nimetoboa... ila duh alipata ajali ya gari ukawa mwisho wake pumzika kwa amani mwamba mtoto wako Jennifer nipo nae kwangu
 
Inahuzunisha sana ๐Ÿ˜ฃ
 
๐ŸฅฒMwamba tulitoka mbali kidogo ila chuo alianza kujiingiza kweny mambo ya hovyo mara kubet yaani sijamuelewa na home kwao najulikana na kwetu anajulikana..

Tulivyomaliza akabaki hapa mi nikarudi home kidogo maana kuna shughuli nilienda kusimamia ,baadae msela sijui alienda wapi mi nikapata kazi hapa ,nilimtafuta nikaambiwa karudi mkoani.

Mungu si Athumani nimekutana na jamaa mwaka Jana akaniambia msela kama mtu wa Mungu sana kabadilika ๐Ÿ™...
 
Leo ktk kuangalia TV, nikamuona Ester Chabruma, kocha msaidizi wa timu ya wanawake under 18 CECAFA. Nikamkumbuka mdogo wake, rafiki, mwana, mshkaji, msela wa utotoni tumepiga boli pamoja, utundu wa shule pamoja... dah.
Mbele yako nyuma yetu swahiba.
 
Mi mshikaji tumeanza nae utoton tulipanga maisha yetu rasmi tukiwa darasa la 5. Mungu alitusaidia sana kwa kuwa tulienda kula kiapo pamoja kanisan. Tulifanya kila kitu pamoja na mpaka nyumba za kuish na za biashara na mpaka tulishaandaa eneo tutakapoish baada ya kufikisha miaka 70. Lakin Mwenyezi Mungu kwa mapenz yake alimchukua bila kuaga. Hilo donda halijawah kupona. Cku hiz the way Ninavyoiona dunia ni tofauti kabisa na huko nyuma. We will meet again on the other side bro. RiP
 
Frank ndio rafiki yangu wa kweli tulikutana shule sekondari ila alikuja kuwa kama ndugu japo utaftaji wa maisha umetuweka mbali ila bado najivunia kuwa nae. Nahis mwingine atakuwa ticha wangu huyu nitamuelezea siku nyingne
 
Ninao wengi nakutana nao kila stage ya kupambana.

Ambaye yuko outstanding ni yule tuliyekutana naye Advance, tukaenda Chuo wote na sasa tupo mtaani pamoja
 
Yupo anaitwa Mwapongo
 
Yupo anaitwa Mwapongo
 
Alipitiwa na usingizi ndio akakosa kufanya mtihani? Usingizi wa kawaida au ndio Shangazi wa kulaumiwa?

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Izack
He was more than a friend




Miaka miwili ya advance ilikuwa km miezi tu kutokana na uswahiba wetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ