Kama raia wa Tanzania mwenye kipato cha kawaida au cha chini, kumiliki ardhi au nyumba ni mtihani mgumu unao hitaji maarifa mengi na hesabu kali. Kadri siku zinavyo zidi kusonga, bei ya ardhi nchini inazidi kupanda pasipo kuwa na udhibiti maalumu. Bei ya soko imetawala, ikiwa watu wana uhuru wa kujibunia thamani ya ardhi pasipo muongozo wowote wala vigezo vya kutamka bei husika.
Bei ya upangaji vivo hivyo, ni ghali. Ilhali ulizingatia hali ya mapango yenyewe hayaendani na gharama hizo. Wengi wetu tunao anza maisha hulazimika kupanga nyumba au kununua viwanja katika maeneo ya mbali ni Miji, kwakuwa ndipo penye unafuu wa bei. Japo hilo nalo ni mtego, mana tunaishia kuteseka na kero za usafiri na mahitaji mengi ya kijamii kama upatikanaji wa shule, hospitali, vyombo vya usalama na ofisi za serikali. Inamuhitaji mtu kusafiri umbali mrefu kuweza kufika kazini au hata kufata huduma za kijamii.
Katika wastani wa Watanzania 10, basi 7 kati yao wanakaa zaidi ya Kilometa 25 kutoka mahali pake pa kazi au shule. Kwa mantinki hiyo, mtu anahitajika kusafiri umbali wa Kilometa 50 kila siku ili kwenda kutafuta rizki ya kijikimu. Vivyo hivyo kwa wanafunzi na wagonjwa, nao hulazimika kusafiir umbali mrefu kusaka huduma hizo.
Kwa sasa, viwanja maeneo yenye majina mjini ni kuanzia Milioni 15 hadi kufikia Bilioni. Na viwanja hivi vingi, sio vikubwa, kwakuwa huwa takribani mita za mraba 450 hadi 800. Vichache sana utakuta vimezidi mita za mraba 1,000 kwa maeneo mengi ya mijini na maeneo maarufu kama vile Masaki, Msasani, Mikocheni, Upanga, Mbezi Beach, Mbweni, Kijitonyama, Kinondoni, Goba, Kijichi, Kimara, Segerea, Kinyerezi huko hakushikiki.
Serikali imejaribu kufanya miradi ya kujenga nyumba za nafuu kwa lengo la kuuza nyumba hizo kwa raia wenye kima cha chini au cha kati lakini zoezi hilo limeangukia pua kwakuwa nyumba hizo zinakuwa bei kubwa sana kulingana na uwezo wa walengwa hao. Mwananchi wa kawaida hawezi kununua nyumba kwa bei kubwa ukizingatia bei zinaanzia Milioni 80 hadi 300.
Mashirika ya serikali kama NHC, TBA na NSSF wameanzisha miradi hiyo lakini hujenga nyumba kwa gharama na kupelekea kutaka kuziuaza kwa bei kubwa ili kuweza kupata faida. Hili swala hupelekea miradi hiyo kushindwa kufanikiwa na nyumba hizo kubaki wazi au kununuliwa na matajiri ambapo kimsingi sio lengo la mashirika hayo.
Baadhi ya miradi hiiyo imeenda mbali hata kuuza nyumba hizo kwa malipo ya awamu na sio mkupuo wa mara moja kama ilivyo zoeleka, lakini shida ipo pale pale-BEI. Kwa mfano, kuna mradi wa shirika moja wapo, sitoutaja ila upo hapo Dar es salaam. Unaambiwa bei ya nyumba ni Mil.148 kwa kulipia kwa mkupuo lakini kwa awamu nyumba ni Milioni Tshs.250,361, 112.79/=. Na malipo ya awamu ni 10% ya bei halisi ya nyumba 148m, kufuatiwa na malipo ya kila mwezi kwa miaka 15 ya Tshs.1,390,895.07/=. Ukiangalia wastani wa wananchi wenye uwezo wa kununua hiyo nyumba kwa masharti hayo ni wachache. Kwahiyo lengo la kusema walengwa ni watu wenye kima cha chini au kati linakuwa la kufikirika na sio la uhalisia. Lakini hata kwa mashirika pia, inakuwa ni changamoto kuuza nyumba hizo kwa faida kwakuwa bei zake zinakuwa juu sana tofauti na thamani yake halisi.
Kwa mawazo yangu, taifa letu linaweza kujikwamua na janga hili kwa kuboresha sera na sheria za ununuzi wa ardhi na umiliki wa nyumba kwa kudhibiti bei za maeneo ili kuweza kucontrol bei ya masoko. Hili linasaidia kupunguza uholela wa watu kujipangia bei zisizo na uhalisia kwa kivuli cha bei ya soko.
Vivyo hivyo, mazingira ya uwekezaji yangeboreshwa ili kuwezesha mashirika binafsi kuwekeza katika ujenzi wa nyumba za bei nafuu. Mashirika binafsi yangefanikiwa kwakuwa yangejenga nyumba hizo kwa ubora na usasa unatakiwa lakini kwa kuzingatia gharama za ujenzi, na hatimaye mashirika hayo yangeweza kuuza nyumba hizo kwa bei yenye unafuu. Hili lingetusaidia walengwa wa miradi kupataka umiliki wa yumba kwa bei nafuu. Ukiangalia nchi jirani kama Kenya na Afrika ya Kusini wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuendesha miradi kwa uwekezaji wa mashirika ya binafsi na sio serikali, na kwa kiasi kikubwa wameweza kutanabaisha bei ya ardhi na nyumba ili wananchi wao wengi wanaweza kumiliki ardhi au nyumba kwa kuzingatia kipato chao.
Lakini pia, suala jigine la kuzingatia ni uboreshaji wa miundo mbinu yetu ili kupunguza adha ya Usafiri. Watanzania wengi tunatumia muda mwingi barabarani kwene foleni, kwenda makazini na kurudu nyumbani. Kwenda kutafuta elimu na huduma za kijamii. Serikali iruhusu sekta binafsı kuwekeza na kuendesha miradi ya usaifrishaji kama vile UDART (Mwendokasi) kwa huduma ya uhakika, Serikali isiishie kwene usafiri wa mabasi ya mwendo kasi bali hata treni za ndani ya miji kama ilivyo kwa nchi za wenzetu.
Hili suala litaruhusu ushindani kati ya utoaji huduma lakini vilevile litatoa wigo mpana wa machaguo kwa wananchi katika usafiri upi unafaa kwa mahitaji binafsi. Hili litapunguza athari ya kilio cha wengi wetu kukaa mbali kwakuwa miunfi mbinu itakuwa imerahisisha mtu kufika kwa haraka kutoka sehemu moja kwenda nyingine lakini vilevile, imepunguza muda tunatotumia au kupoteza katika usaifir ili tutumie muda huo katika maswala mengine ya kimaendeleo au hata kupumzika.
Vilevile, kutengeneza miundombinu ya kupanua miji yetu kwa kupeleka huduma nje ya mji ili kupunguza msongamano mijini. Hili likiongezewa na miundo mbinu mizuri na ya kısasa ya upangaji wa miji na vijiji. Hili swala litaleta tija na kuongeza thamani kwa maeneo mengi yanayoonekana ni makazi ya watu wa chini kwakuwa ni mbali na miji, huduma za kijamii na maofisi ya usalama na huduma za kiserikali. Kufanyika kwa hili jambo kutapunguza kwa kiasi kikubwa kupunguza misongamano katika maeneo machache ambapo huduma ndo zinapatikana kwa sasa.
Hii itarandana na sera za nchi za kisasa kwa kuleta usawa wa maeneo mengi na kutoa ile dhana ya kwamba kuna maeneo ambayo ni bora na yenye thamani kuzidi menzake kwakuwa tu yako karibu na miji na huduma mbalimbali za mahitaji yetu ya kila siku. Kila sehemu itakuwa iko karibu na huduma hizo kwahiyo kila sehemu itakuwa na thamani. Na hakuna sehemu itaonekana ni mbali kwakuwa kila huduma itakuwa inapatikana kwa urahisi na wananchi tutakuwa katika hali ya kiuweza kuwekeza katikka unuzi wa ardhi na nyumba kwa unafuu.

Upvote
2