Nimeangalia rasimu ya pili ya katiba mpya sijaona popote pale walipozungumzia swala la umiliki wa ardhi. Binasfi ninalichukulia swala la umiliki wa ardhi kama ishu muhimu ambayo ilitakiwa kuwepo/kuwekwa wazi ndani ya katiba mpya.
Kwa katiba ya sasa ardhi ni mali ya serikali. Kauli hii imewafanya viongozi wajichukulie ardhi kama watakavyo na kutuacha sisi wengine mikono mitupu.
Viongozi wa serikali wamekuwa na maheka na maheka ya ardhi waliojimilikisha. Wananchi tuliosalia hata kama tuna ardhi basi ardhi hiyo iko rehani kutokana na ukilitimba na mlolongo mrefu wa kumilikisha ardhi hiyo. Siku yeyote ile unaweza kusikia ardhi ambayo umekuwa ukiitumia miaka na miaka ni mali ya kiongozi furani. Ukifatilia ni kweli kiongoizi huyo ana hati zote. wewe una barua ya mwenyekiti wa kijiji/kitongoji ambaye haina nguvu kiasi cha kukupatia haki yako pale unapodhurumiwa.
Natamani isiwe tena mali ya serikali. Natamani katiba mpya iseme kwamba ardhi ni mali ya wanachi.
Wewe unasemaje juu ya umiliki wa ardhi?