Umiliki wa Ardhi nisaidieni

Umiliki wa Ardhi nisaidieni

Zabron Erasto

Member
Joined
May 29, 2011
Posts
47
Reaction score
3
wanajukwaa naomba msaada wa taratibu za kupata HATI MILIKI ya ardhi kwa hekari 15 Pia na sheria ya ardhi kuhusu hati miliki.
 
Unataka Hatimiliki ipi kwani kuna HATIMILIKI YA KIMILA inayotolewa kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi No. 5 ya Mwaka 1999 (Kumbuka hatimiliki hii hutolewa na serikali ya Kijiji). Ya pili ni hatimilki ya inayotelewa kwenye ardhi kuu (general land) ambayo ipo chini ya Kamishna wa Ardhi. Hatimiliki hii inaitwa (granted right of occupancy) hatimiliki ya kiserikali inatolewa kwa mujibu wa Sheria N0.4 ya Ardhi ya Mwaka 1999 kwa kuzangatia miongozo na kanuni zake za mwaka 2001.
 
Ahsante ndugu nataka hati miliki inayotolewa kwenye ardhi kuu(general land)
 
Bila shaka hilo ni shamba, Je lipo kijijini kwa maana lipo chini ya Halmashauri ya kijiji. Kama ndiyo hivyo basi hatua za uhawilishaji zinahitajika.
 
Yaani ndugu yangu suala la kupata hati milki kutoka ardhi kuu ni kizungu mkuti. Haswa haswa kama ni hapa Dar si mchezo. Nimeanza process ya hati yangu mwaka jana mwezi wa tatu mpaka hivi naandika bado sijaipata hiyo hati. Kama unaanzia manispaa ya Temeke, duuh ni balaa. Mara utaambiwa file imepotea, mara kalete cheti cha kuzaliwa, ukipeleka wanakuambia affidavit inahitajika basi tuu ni usumbufu wa hatari. Kuna wamama pale ofisi ya masijala, heri ukutane na dubu anaweza kukuhurumia kuliko wale wamama. Ila kama ni mtoa rushwa, utaipata hata ndani ya siku 3.
Kuna jirani yangu alienda kuprocess hati hiyo hiyo hivi tunaongea alishaipata siku nyingi ingawa hata kupima hilo eneo mimi ndo niligharimia. So my friend, jiandae kisaikolojia kabla hujakutana na watumishi wa ardhi.
All the best
 
samahani naomba kujua vitu vya kuzingatia kabla ya kufuhatilia hizo hati miliki ya kimila na ya ardhi kuu (general land),pia taratibu zake kwa ujumla.
 
mimi niko arusha na eneo langu liko ndani ya jiji,ninahitaji kupata hati miliki naomba msaada wa ushauri.
 
mimi niko arusha na eneo langu liko ndani ya jiji,ninahitaji kupata hati miliki naomba msaada wa ushauri.

mkulu ni maeneo gani ya jiji na ulinunua lini?hapo tunaweza tukaendelea maana maeneo mengi wanayoyaita general land au planned area yanahati au wewe hujadai yako au ni maeneo ya sekei nini?
 
eneo linatakiwa liwe limepimwa na ramani yake ipate kibali cha Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani! baada ya hapo Afisa ardhi atahitajika kufanya ukaguzi ili kujilizisha,then utatakiwa kulipia gharama zifuatazo fee for certificate 1600000,deed plan fee 6000,survey fee kama bado,land rent,stamp duty na registration fee
kisha utaandaliwa aknowledgement of payment utasign then utaandaliwa certificate ambayo u/itapelekwa kwa commisner for lands na kisha msajili wa hati
 
hekari 15 mjini?sina hakika kama it is possible! maana ni sqm 150,000 na matumizi ake ni yapi?
 
Wakuu kuna tofauti gani kati ya HATIMILIKI ya KIMILA na HATIMILI KUU,,,,kwa maana ya matumizi yake,,,!
 
Wakuu kuna tofauti gani kati ya HATIMILIKI ya KIMILA na HATIMILI KUU,,,,kwa maana ya matumizi yake,,,!

Hati miliki ni Certificate of right of occupancy hii ni legal instrument na proof ya umiliki wako wa intrest fulani katika ardhi!!wakati haki miliki ama Right of Occupancy ni umiliki (ownership na possesion) juu ya ardhi ambayo kwayo hati hutolewa. Ahsante
 
Hati miliki ya kimila inatolewa kwa ardhi za vijiji na hati miliki kuu hutolewa kwa maeneo ya mijini!!! Na hizi zinasimamiwa na sheria mbili tofauti!hati miliki za kimila zinatolewa na halmashauri za vijiji wakati za general land zinatolewa na kamishna wa ardhi!!
 
Hati miliki ya kimila inatolewa kwa ardhi za vijiji na hati miliki kuu hutolewa kwa maeneo ya mijini!!! Na hizi zinasimamiwa na sheria mbili tofauti!hati miliki za kimila zinatolewa na halmashauri za vijiji wakati za general land zinatolewa na kamishna wa ardhi!!

Mkuu,,nakushukuru sana kwa Ufafanuzi huu Endelea kubarikiwa,,,,!!
 
Back
Top Bottom