Yaani ndugu yangu suala la kupata hati milki kutoka ardhi kuu ni kizungu mkuti. Haswa haswa kama ni hapa Dar si mchezo. Nimeanza process ya hati yangu mwaka jana mwezi wa tatu mpaka hivi naandika bado sijaipata hiyo hati. Kama unaanzia manispaa ya Temeke, duuh ni balaa. Mara utaambiwa file imepotea, mara kalete cheti cha kuzaliwa, ukipeleka wanakuambia affidavit inahitajika basi tuu ni usumbufu wa hatari. Kuna wamama pale ofisi ya masijala, heri ukutane na dubu anaweza kukuhurumia kuliko wale wamama. Ila kama ni mtoa rushwa, utaipata hata ndani ya siku 3.
Kuna jirani yangu alienda kuprocess hati hiyo hiyo hivi tunaongea alishaipata siku nyingi ingawa hata kupima hilo eneo mimi ndo niligharimia. So my friend, jiandae kisaikolojia kabla hujakutana na watumishi wa ardhi.
All the best