Kama msichana umeolewa na mwanaume ambaye tayari umemkuta na vitu vyake, I mean may be umemkuta na mali kama Nyumba, magari na vitu kama hivyo, na kila kitu kipo kwenye jina lake. je kwa kisheria hivyo vitu vitahesabika vya wote kama mmeoana? Au kuna uwezekano wa yy kubadili jina hati zote na kuandika jina lake na mkewe?
Nahitaji kujua kama hii sheria ipo.
Kama msichana umeolewa na mwanaume ambaye tayari umemkuta na vitu vyake, I mean may be umemkuta na mali kama Nyumba, magari na vitu kama hivyo, na kila kitu kipo kwenye jina lake. je kwa kisheria hivyo vitu vitahesabika vya wote kama mmeoana? Au kuna uwezekano wa yy kubadili jina hati zote na kuandika jina lake na mkewe?
Nahitaji kujua kama hii sheria ipo.
1. Hivi mkifunga ndoa: baada ya wiki 2 ikavunjika na mmali yote ni ya baba na mke amekuwa tu mama wa nyumbani, je hapo ina maana mke hatapewa chochote kisheria?
2. Watoto/Mke wa nyumba ndogo je atakuwa na sauti gani gatika mali ya familia?
Anytime Msanii.Uskonde wala nini..just shoot!WOS
nakuja kusoma sheria kwako
ila nina vijiasignment fulni naomba unisaidie maana nipo majalala hapa sana tu. je upo tayari kunsaidia?
please can you measure
Cicero's advise vis-a-vis provisions of the LAND ACT on DISPOSITIONS
unayo introduction
of the philosophical conception of 'DUTY' or 'OBLIGATION' and why the
moral obligation to DUTY overrides EXPEDIENCE [Utility] yake?
kama huna niputumie kwenye PM
Ahsante WoS kwa maelezo yako ya kisheria.Nitajaribu kukujibu kwa kifupi kama ifuatavyo:
Sheria ya Ndoa ya 1971( LMA/Act no.5/1971) inaweka utaratibu wa kuwa na mali baina ya wanandoa kama ifuatavyo:- mali ya pamoja kwa maana wote wamechangia kuipata na wana haki nayo.Vilevile inaruhusu wanandoa kuwa na mali binafsi - kwa maana mtu anaweza kuwa na mali aliyoipata kabla, au aliyorithishwa n.k. in short siyo joint property.Uthibitisho wa mali ni pamoja na hati yenye jina la mhusika.KUOANA HAKUBADILI AUTOMATICALLY HIZO MALI NA KUZIFANYA JOINT UNLESS MUWE NA MAKUBALIANO YA HIVYO.Huu ndiyo msimamo wa kisheria.
kwanza kisheria hamwezi kuvunja ndoa kwa talaka ya kimahakama kama hamjakaa miaka miwili minimum.( Unless kuwe na sababu kubwa sana kama non-consumation of marriage na hii itafanya hiyo ndoa iwe batili tangia mwanzo.Kwa msingi huo hakuna cha kugawana mali.. labda mgawane zile zawadi mlizopewa wakati wa harusi ( tena za send-off zinaweza kuwa za bibi harusi mwenyewe..bwana harusi hazimhusu).