joshydama
JF-Expert Member
- May 10, 2016
- 4,623
- 5,039
Habazi za mchana waungwana wa JF? Ni matumaini yangu kwamba wote hamjambo humu ndani.
Waungwana nimependa kuleta huu uzi mzuri kwenu nyie kwa lengo la kuwasaidia vijana wenzangu kuhusu suala la umiliki wa mali wakati mkiwa katika maisha ya uchumba na kila mmoja akiwa amechuma mali zake na mnatarajia kufunga ndoa. Pia ningependa kuelezea umiliki wa mali katika maisha ndoa.
Waungwana kama mjuavyo kila mtu ana haki ya kumiliki mali kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ibara ya 24(1). Mali inaweza kuwa ni Ardhi( kiwanja), nyumba, n.k. katiba inaposema kila mtu inamaanisha kwamba ni mtu mzima yeyote mwenye miaka 18 na zaidi(majority age). Kwa mantiki hiyo haibagi mwanamke kutomiliki mali. Ingawa kuna baadhi ya makabila huwa yanawanyima wanawake kumiliki mali kutokana na mila zao mfano Wakurya, wachaga na Wahaya. Mila zinazomnyima mwanamke asimiliki mali zipo kinyume na katiba ya JMT. Hivyo hizo mila hazifai hata kidogo.
Baada ya utambuzi ni wapi tunapata haki ya kumiliki mali naomba nizungumzie umiliki wa mali kwa wachumba kabla ya ndoa na katika maisha ya ndoa.
I. Umiliki wa mali kwa wachumba kabla ya ndoa.
- kama tulivyoona hapo juu ni kwamba kila mmoja anyone haki ya kumiliki mali. Hivyo basi kijana wa kiume au wa kike ana haki ya kumiliki mali kabla ya ndoa.
Ni nini kifanyike kulinda mali zako kabla ya kufunga ndoa ili kuepuka migogoro ya kisheria ya hapa na pale.
- Kama unamiliki mali zako binafsi mfano nyumba, mashamba, viwanja, magari na unataraji au una nia ya kufunga ndoa na mwenza wako mnatakiwa kuandaa mkataba wa kisheria (prenuptial agreement) ambao utabainisha na kuorodhesha mali zote za kila mmoja alizochuma na pia pawepo na kifungu dhahiri kinachoeleza kwamba mali zilizochumwa na mwenza mmoja kabla ya ndoa ni za kwake peke yake na hazimhusu mwenza mwingine.
Aidha, huo mkataba unatakiwa uweke wazi haki na majukumu ya wahusika katika mkataba huo pale ambapo mtaingia katika maisha ya ndoa.
Ni nini lengo la huu mkataba?
-Lengo kubwa ni kuzuia mgogoro wa mali inapotokea suala la kifo au talaka au pale unapokuwa una shida yako binafsi na unatakiwa kuuza au kuchukua mkopo kupitia hizo mali zako.
- Kumbuka kwa sasa pamekuwa na limbi kubwa la watu kutalakiana na mwisho wa siku kutaka kugawana mali tena katika usawa wa 50% kwa 50%.
- Hivyo basi pakiwepo kwa huo mkataba utazuia migogoro ya hapa na pale.
II. Umiliki wa Mali ndani ya Maisha ya Ndoa
- Baada ya kuingia katika maisha ya ndoa tambua kwamba mali mtakazochuma ni mali ya wanandoa wote wawili hata kama mwanaume au mwanamke atachuma kwa jitihada zake yeye mwenyewe hata kama utaandika kwa jina lako wewe tambua kwamba hiyo mali itakuwa ni mali ya wanandoa wote wawili au mali ya familia labda tu pawepo na mkataba kama nilivyoeleza hapo juu.
- Bila kuwepo na mkataba huo basi kutakuwa na dhanio kwamba hizo mali ni za familia( Matrimonial property or asset) hata kama mwanamke au mwanaume alikukuta na mali ambazo ulikuwa umechuma peke yako.
#Kadhalika, baada ya ndoa mnaweza kuamua kumiliki mali kwa pamoja(Joint ownership). Huu umiliki wa mali kwa pamoja unatambulika kisheria na ni mzuri sana kwa sababu kama mnamiliki kwa pamoja. Pindi mmoja wenu anapokufa malizo zote humilikiwa na aliyepo hai( Right of survivorship).
-Pia mtu mwingine hatakuwa na haki nazo ni mpaka pale tu wamiliki wote wa mali hizo mtakapokuwa hampo Duniani au mmefariki Dunia.
- Katika umiliki huu ni kwamba wote mnakuwa na hisa sawa( equal shares of ownership of the property)
-Hapa inabidi pawepo na mkataba unaonesha kwamba mnamiliki mali kwa pamoja.
#Mbali na umiliki ulioelezewa hapo juu, kuna umiliki unaitwa tenancy in common. Huu umiliki ni kinyume chake na huo umiliki wa pamoja (joint ownership). Katika umiliki huu, siyo lazima muwe na hisa sawa za umiliki wa mali bali mmjoa anaweza kuwa anamiliki 1/3 na mwingine 2/3 ya mali hiyo. Katika umiliki huu ni kwamba pindi mmoja wenu akifa hisa (share) yake itaenda kwa mtu aliyemuandika kwenye wosia wake. Pia unaweza uza hisa yako bila matatizo yoyote.
# Kadhalika ni ngumu sana kuhamisha maslahi ya mali ya familia kwenda kwa mtu mwingine bila kuwepo na ridha mwenza (Spousal Consent) mfano huwezi ukapewa mkopo na benki kwa kuweka rehani mali ya familia bila kuwepo na nyaraka ya kisheria inaitwa ridhaa mwenza( Spousal Consent).
#Karibuni kwa michango, maswali pamoja na nyongeza.
#Imeandaliwa na mshauri wa masuala ya kisheria katika masuala yafuatayo:-
Ahsanteni sana.

- Ndoa
- Ardhi
Ahsanteni sana.