Umiliki wa mali kwa wanandoa

Umiliki wa mali kwa wanandoa

Jstar1

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2019
Posts
1,391
Reaction score
1,347
Naombeni kuuliza kuhusu umiliki wa mali kwa wanandoa endapo watatengana, mfano,

Mke kama amekuta mmewe tiari kuna mali anamiliki mfano, nyumba je ikitokea mmetengana na hamkua na watoto mke atapata asilimia ngapi ya nyumba au mali na je kipi kitaprove kua hii mali kaikuta au wataoanisha cheti cha ndoa na hati ya nyumba imetoka lini?

Na je kama mmepambana wote kujenga, ikitokea mmetengana atapata asilimia ngapi na kitaprove kua mmjenga wote na je ukisema kaikuta na kama mna watoto inakuaje?

Najua humu kuna wajuvi wengi wa mambo hili ni dogo kwenu naomba mtririke
 
Mi sio mwanasheria.,
Ila nasikia hata kama nyumba kaikuta umejenga wewe maadamu tu ni 'matrimonial home'..50/50 inahusika..

i js wonder how do u sleep at night kuchukua kitu ambacho hujakifanyia kazi
 
Hizo sheria zenu za kidunia na dhulma, sheria ya kiislaam insema mtakapo achana achanenei kwa wema

Ukimuacha mwenza wako inatakiwa ukampa kitoka nyumba, yaani umpe chochote kile cha kumliwaza huko anako kwenda sio mgawane 50/50 hapana hiyo

Ila kama mmejenga pamoja au mmefanya biashara pamoja hapo share inahusika lakini sio mali uchume baba au kachuma mama mkiachana mgawane 50/50 hakuna hiyo kwenye dini tukufu ya kiislam, wajuvi zaidi w dini yetu watakuja hapa watafafanua zaidi

Allahu alaam
 
Oa mke ili mali zako ziwe salama ukioa slay kwini umeisha
Hakuna kuoa mkuu.. tunaishi kam wasela kwao hakuna kufahamika wala kwetu ndio mwalobaini wa kuepuka mgao.. uzuri mabinti wana jirahisisha kukaa kwa wasela kirahisi rahisi, unampata leo kesho anahamia magetoni, akizingua anaondoka kama alivyokuja 😀😀😀
 
Hakuna kuoa mkuu.. tunaishi kam wasela kwao hakuna kufahamika wala kwetu ndio mwalobaini wa kuepuka mgao.. uzuri mabinti wana jirahisisha kukaa kwa wasela kirahisi rahisi, unampata leo kesho anahamia magetoni, akizingua anaondoka kama alivyokuja 😀😀😀
Heheheheh tunakutana kimjinimjini...tunaachana kimjinimjini
 
Kwa Mali alizokukuta nazo mwanamke hz hazimuhusu! Mali mlizochuma wote hizo ni 50/50
Kama mna watoto mahakama itaangalia Nani Kati ya mama au baba abaki na watoto kwa kuzingatia umri na usalama au ustawi wa watoto ! Mahitaji ya watoto baba utaendelea kuhudumia kama kawaida kwa wastani wa shs USD 1 kwa siku kwa kila mtoto! Hiyo ni nje ya mahitaji ya shule afya mavazi nk
 
Back
Top Bottom