Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Hii ni kutoka kwa kamati ya miss Tanzania kwamba kuepusha utata wa umri na udanganyifu kamati imeamua kuanzia sasa warembo wote wanaotaka kugombea taji hilo maarufu waonyeshe pia na kadi zao za kliniki
Yaani baada ya sekeseke la binti mtemvu ndio kamati imekuja na ufumbuzi huu...!
======================================================================================================================
CHANZO: Mwananchi
Yaani baada ya sekeseke la binti mtemvu ndio kamati imekuja na ufumbuzi huu...!
======================================================================================================================
Kwa ufupi
Alisema kuwa dunia ya leo imebadilika na kamwe huwezi kumuamini mtu moja kwa moja na kwa kujua hilo, tumeamua kuchukua tahadhari mapema.
Katika hali ya kuchukua ahadhari zaidi, waandaaji wa mashindano ya kumsaka Miss Universe Tanzania 2014, wameamua kutumia kadi za kliniki za watoto kujiridhisha katika suala la kupata umri halisi wa warembo wao.
Mratibu wa mashindano hayo, Mwanakombo Salim alisema kuwa warembo hao 12, watakaochuana Ijumaa wamepewa sharti hilo ili kuepuka malumbano ya umri.
Mwanakombo alisema suala la umri ni nyeti na mbali ya kutumia vyeti vya kuzaliwa, wao wameamua kwenda mbali zaidi kwa kutaka kadi zao za kliniki za utotoni.
"Miss Universe anatakiwa kuwa na vigezo mbalimbali pamoja na umri uziozidi miaka 25, asiwe ameolewa wala kuzaa mtoto, lakini hivi karibuni kumetokea malumbano ya umri kwa wenzetu, sitaki kuingia huko, sisi tumeamua kwenda mbali zaidi na warembo wameambia hayo na tunashuru hakuna tatizo mpaka sasa," alisema Mwanakombo.
Alisema kuwa dunia ya leo imebadilika na kamwe huwezi kumuamini mtu moja kwa moja na kwa kujua hilo, tumeamua kuchukua tahadhari mapema.
Awali Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi Tsehai alisema kuwa mwaka huu wamepanua wigo wa mashindano yao kwa kumshirikisha mrembo kutoka Zanzibar. Maria alimtaja mrembo huyo kuwa ni Zahra Bedel ambaye tayari yupo kambini.
Warembo wengine ambao wameanza kambi kwa ajili ya mashindano hayo ni Christine Halamga, Amina Sangalwe, Faith Felix, Belinda Lugenge, Magreth Geddy na Carolyne Benard ambao wote wanatoka Dar es Salaam.
Wegine ni Nale Boniface, Neema John (Dar es Salaam), Zahra Bedel (Zanzibar), Lucy Charles, Faudhia Haruna (Mwanza) na Atukuzwe Fabian kutoka Mbeya.
Alisema kuwa maandalizi ya mashindano hayo yamekwisha kamilika na mshindi atachukua taji kutoka kwa Miss Universe anayemaliza muda wake, Betty Boniface ambaye kwa sasa anafanyakazi Azam Televisheni.
CHANZO: Mwananchi