Pre GE2025 Ummy aumbuliwa, ajikuta akisifia kwa takwimu za zamani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
59,045
Reaction score
94,974
Kutoka mtandao wa X, kizuri Kula na mwenzio, naweka hapa ili wapiga zumari wajifunze Namna ya kumsifia unayempenda bila kujidhalilisha. Kumbuka technology haiongopi. Tunadanganya kwa faida ya Nani? Rais Samia kataa sifa hizi za kipumbavu. Pokea zile unazostahili.

====

Bandiko hili kwa hisani ya Onesmo Mushi wa X.

Mhe. Waziri @ummymwalimu , naomba unisaidie ufafanuzi kidogo kuhusu hii taarifa kwamba Rais Samia amepunguza “vifo vya wakina mama wajawazito kwa asilimia 80% kutoka vifo 556 mpaka vifo 104” inanipa ukakasi.

Kwa mujibu wa Tanzania in Figures ya Shirika la Takwimu Tanzania (NBS, 2017), Rais Magufuli alipoingia madarakani 2016, idadi ya vifo vya wakina mama wajawazito ilikuwa 556/100,000, idadi ambayo ilikuwepo tangu mwaka 2004 (de.tzembassy.go.tz/uploads/Tanzan… )

Demographic and Health survey ya Tanzania mwaka 2022 inasema mpaka kufikia muda survey 2021, uwiano wa vifo vya wamama wajawazito ilikuwa 104/100,000 huku confidence level ikirange kati ya vifo 59-149 (nbs.go.tz/nbs/takwimu/dh… )

Kwa mantiki hii, wakati Rais @SuluhuSamia anaingia madarakani mwaka 2021, uwiano wa vifo vya wamama wajawazito ulikuwa at most 149/100,000.

Sasa Mhe., hii “asilimia 80%” aliyoipunguza Rais @SuluhuSamia unayomnadi nayo hapa ni ipi?🤔

Kwa nini unasema amepunguza kutoka vifo “556” wakati takwimu zinasema alipoingia madarakani tayari tulikuwa na vifo chini ya 200?🤔
🙏🏿🙏🏿

View: https://twitter.com/EduTalkTz/status/1787687124382175507?t=lcr1OJ8bZAU86kQ_79RBdg&s=19

Ummy hana muda wa kusoma takwimu zaidi ya kufukuzia dili
 
Kwani ikitamwa "serikali imefanya hiki na kile" kuna ubaya gani. Hii tabia aliianzisha JPM , kupenda sifa na kuabudiwa, leo naona kila mtu anaimba mapambio, ni kusifu, kusujudu na kuabudu kwa raisi. Ona sasa takwimu zinamuumbua.
Anatakiwa kuwajibika kwa kujihuzulu haraka sn
 
Wanadhani watanzania wa sasa Bado ni mang'ombe! Hatufuatilii takwimu!?

Kila uchwao!... Wakilala wakiamka wanawaza namna Gani wata mpamba huyo mama yao!!!
 
Ummy ni mwanasiasa. Elewa tabia za wanasiasa hutopata shida
 
Back
Top Bottom