Ummy Mwalimu amewashukuru Watumishi wa Sekta ya Afya na Watanzania kwa ushirikiano alioupata kipindi cha Uwaziri wake

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
"Ninawashukuru watumishi wa sekta ya Afya na Maendeleo ya jamii wa ngazi zote kwa ushirikiano mzuri walionipatia katika kutekeleza majukumu Nawashukuru kwa imani na upendo wao mkubwa kwangu.Siku zote wamekuwa wakiniamini na kuniheshimu licha ya kuwa sio mwanataaluma wa Afya."

"Kwa unyenyekevu mkubwa, ninamshukuru sana Mhe Rais Dkt Magufuli kwa kuniamini kuwa msaidizi wake wa kusimamia sekta ya Afya na Maendeleo ya Jamii katika kipindi hiki. Asante sana Rais Magufuli. Hakika ulikuwa wakati mzuri kwangu. Nimejifunza mengi kutoka kwako"

"Naamini wengi mtakubaliana nami kuwa sekta ya Afya ni moja ya sekta ambazo zimepata mafanikio makubwa katika Utawala wa Awamu ya 5,hii yote ni kutokana na utashi na dhamira ya dhati ya Rais Magufuli ya kutaka kuboresha maisha ya watanzania hususani wa kipato cha chini"

"Katika utekelezaji wa majukumu yangu pia nimepata ushirikiano mzuri kutoka kwa wadau mbalimbali ikiwemo sekta binafsi, mashirika ya kiraia na Wadau wa maendeleo wa ndani na nje ya nchi. Ninawashukuru sana kwa kuchangia mafanikio makubwa tuliyopata katika sekta hii"

"Ninawasihi sana tena sana tuendelee kuwekeza kwenye afya zetu. Ili kulinda na kuimarisha Afya zetu Tuzingatie ulaji wa vyakula unaofaa, kupunguza unywaji wa pombe kupita kiasi, kufanya mazoezi mara kwa mara AfyaNiMtaji"
 
Kwahiyo anautaka tena uwaziri sio.. Aache kujitongozesha.. Kama ipo ipo tu.

Sekta ya afya hovyo kabisa! Waathirika wa ajali ya moto wa Lori la mafuta Morogoro walikufa wengi Sana kwa uduni wa utaalamu na vifaa tiba ktk hospitali ya Muhimbili.

Mtu kaungua ngozi analazwa kwenye kitanda badala ya jokofu. Hovyo kabisa!

Sekta hii bado sana Ummy aache bla bla. Maduka mengi ya MSD yamejazwa makopo na chupa tupu badala ya dawa. Hovyo!

Wagonjwa wa cancer kule Ocean Road Cancer Institute wanakufa kama kuku. Mgonjwa akianza kupewa chemotherapy ujue ndiyo anapewa tiketi ya kifo. Hakuna utaalamu kabisa pale. Full usanii.
 
Back
Top Bottom