Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini, Ummy Mwalimu amewahimiza wananchi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura, ili kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Mhe. Ummy ametoa wito huo, Februari 14, 2025, baada ya kuboresha taarifa zake katika Kituo cha Suji, Mtaa wa Suji, Kata ya Mzingani.
"Nahimiza wananchi wa Tanga Mjini kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao. Pia, kwa wale wanaotarajia kufikisha umri wa miaka 18 mwezi wa 10, wanapaswa kujiandikisha mapema ili wapate vitambulisho vya kupiga kura ambavyo vina faida nyingi, ikiwa ni pamoja na kufungua akaunti benki na kuomba mikopo," alisema Mhe. Ummy.