Ummy Mwalimu: Marburg imeisha rasmi Tanzania

Ummy Mwalimu: Marburg imeisha rasmi Tanzania

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1685714090941.png

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu Ummy Mwalimu leo tarehe 02 Juni 2023 akiwa Bukoba Mkoani Kagera ametangaza kuwa mlipuko wa ugonjwa wa Marburg umekwisha rasmi Tanzania.

“Kwa mujibu wa miongozo ya Shirika la Afya la Duniani (WHO), tangu tulipomruhusu mgonjwa wa mwisho, tulipaswa kuendelea kuchukua hatua za udhibiti ikiwemo ufuatiliaji wa tetesi katika jamii na kuchunguza Wahisiwa wote kwa siku 42 tangu mgonjwa wa mwisho alipopona Virusi vya Marburg, kwa hesabu hizo, ilipofika juzi tarehe 31 Mei 2023, tulifikisha siku 42 tangu mgonjwa wa mwisho kupona Virusi vya Marburg, na hivyo kukidhi vigezo vya WHO vya kutangaza mwisho wa mlipuko wa ugonjwa wa Marburg”

“Nawakumbusha Wananchi wote kuwa, kumalizika kwa mlipuko huu isiwe mwisho wa kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga dhidi ya magonjwa ya kuambukiza kama inavyoelekezwa na Wataalamu wa Afya na kwa Wataalamu wa Afya tuendelee kuchukua tahadhari wakati wote kama miongozo yetu inavyotutaka”
 
Huyu bibi ni muongo, kapima watanzania wote? kuna watu wanaenda kwa waganga wa kienyeji badala ya hospitali
 
Back
Top Bottom