Ummy Mwalimu safisha kwako kwanza

Ummy Mwalimu safisha kwako kwanza

Standards Person

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2021
Posts
672
Reaction score
860
Ummy Mwalimu nakusalimu kwa jina la jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Ndani ya wiki hii umewasimamisha kazi wakurugenzi wawili wapishe uchunguzi kwa ubadhirifu.
Mheshimiwa Ummy kwakuwa umekuwa Waziri wa TAMISEMI naomba sasa umshughulikie Mkurugenzi wa Halmashauri yako ya Tanga.

Kwakua uliwasimamisha wakurugenzi hao kwakupewa taarifa na wananchi sasa unakumbushwa kwamba wananchi wa Tanga walishakupa malalamiko maranyingi juu ya matumizi mabaya ya ofisi ya mkurugenzi na ukawa unaogopa kutoa taarifa kwani ulikua unahofia kupokonywa tonge kwenye uchaguzi mkuu. Mkurugenzi wako amepokonya watu viwanja vyao amboni,kichangani,masiwani na maeneo ya airport. Ameuza kiwanja kimoja kwa zaidi ya mtu mmoja akisaidiana na watu wa ardhi hasa jamaa mmoja anayeitwa Tony.

Pia wamewauzia wananchi viwanja marambili wakidai eti wananchi ni wavamizi. Kuna kijigari cha watu wa mipango miji kinazungukia vibali vya ujenzi yani wanakula rushwa kama hawapo Tanzania. Watu wameumizwa kwa kuporwa viwanja vyao na wengine wamekufa na mkuu wa wilaya amefanya mkutano na wanatanga akaunda kamati lakini kilichobainika hakijulikani. Hawezi hata kumuuliza kitu mkurugenzi

Mkurugenzi huyo nimpigaji na haelewani na watumishi waadilifu. Hata kisa cha kumkataa Sele Bosi aliyekua meya nikwasababu meya sio mpiga dili.Mea anasimama na wananchi wakati mkurugenzi anakikosi chake cha wanyang'anyi na watu wa jinsia nyingine ile

Mkurugenzi huyo amekua mzulumaji lakini Jafo amemlea kilichotokea Mungu kamuondoa huyo mlinzi wake hapo wizarani. Mkurugenzi anajua kuitumia hela maana atakaekuja mbele yake akipiga kelele anamtuliza kwa namna anavyojua. Waandishi wa habari wakiingia wanatoka na bahasha. Kama kunamtu anashida ya hela hata anafanyakazi wizarani akafanye ukaguzi Tanga hatalala njaa.Hata waziri wa ardhi bwana Lukuvi alikuja kwa mbwembwe lakini akaondoka mpoleeeee. Kuja kwa Lukuvi pia ni baada ya wadau wenye uchungu na maendeleo ya Tanga kwenda kulalamika ikulu. Lukuvi aliwaacha wanatanga na maumivu kwani waliendelea kudhulumiwa viwanja.

Kila idara ameharibu kwa ubadhirifu yaani ameacha watu wamekufa kwa kuwadhulumu viwanja vyao wewe Ummy unajua,mkuu wa wilaya anajua na aliunda kamati yake ya uongo na kweli,mkuu wa mkoa ndio amemnyamazia mtu huyo na takukuru ndio wamelala fofofo usingizi wa pono.Ukweli nikwamba mkurugenzi huyo ndio kiongozi mkuu ndani ya halmashauri akiamua hakuna atakayemzuiya sio mkuu wa mkoa wala katibu tawala.

Nimetuma salam kwako kukukumbushatu kwamba ameumiza watu wengi sana hasa waliomkatalia kuiba. Yaani nimafia anaweza kukufanyia zengwe lolote endapo utakataa kuiba nae. Suala la aina nyingine zile za rushwa ndio uaiseme yaani ni fundi na jinsia ke inamchanganya sana

Ummy fagia nyumba yako ni chafu isafishei ina tandabui inanuka uvundo na imejaza nzi ndio watu wanaoijua halmashauri yako wataona unafanyakazi kwa misingi ya haki. Simamisha kazi mbadhirifu huyo nae achunguzwe kisha apelekwe mahakamani umuunganishe na watu wake wa ardhi kina Tony. Mheshimiwa Rais ondoa hawa wasumbufu kwenye halmashauri imekufa,wawekezaji baadhi wamefunga viwanda kila mara wanawafuata kudai michango na sio ya maendeleo ya jamii nikwaajili yao na wapenzi wao

Ummy Fanya maamuzi kwani wewe ni mwanamwema wa Tanga lakini huyo anapita, usimuogopa alikuweka hapo hatakuweka tena atakuja mwingine.

Jana Mh. Rais amesema ng'ombe hanenepi na mfugaji hanenepi. Tanga hawana nafuu na halmashauri inaliwatu
 
Ummy Mwalimu akiwa tamisemi amechukua uamuzi wa kuwasimamisha kazi wakurugenzi wawili kwa ubadhirifu. Amedai amepata taatofa kutoka kwa wananchi. Wananchi kama tulivyokua na jukumu la kutoa taarifa tunamtaarifu Ummy kwamba Mkurugenzi wake Tanga anatumia ofisi vibaya kwa muda mrefu. Ulishapewa taarifa ukawa unasema aambiwe Jafo na Jafo nae akawa ni mtu wakaribu na mkurugenzi hakumfanya chochote zaidi ya kucheka kula pamoja na kumsifia mkurugenzi huyo kila akija Tanga.

Mkurugenzi wako amekua mpigaji kwamuda mrefu na mtumishi yoyote akikataa kupiga nae au akihoji atajikuta matatizoni. Halmashauri yako unaijua imejaa majungu,umbea na ufanisi ndio kidogo.

Watu ambao sio wezi hawatakiwi. Wamempinga aliyekua meya mh.Sele Bosi kwakua sio mwizi.Hamtaki kabisa maana yupo kwaajili ya wananchi. Hataki madiwani wanaojielewa. Ameshapelekwa takukuru lakini hashikiki kwani anajua kuitumia hela.

Anajua kuwatuliza watu waliojuuyake.Mkuu wa mkoa,katibu tawala hawana chakusema kwa mkurugenzi huyo. Hata waziri wa ardhi alifika Tanga akaishia kufungiwa wakafanya kikao cha ndani muda mrefu alipotokea kwa wananchi hakua na jipya. Ameacha migogoro ya ardhi wawekezaji wameporwa maeneo yao huko Amboni wamepewa wengine,wanatanga wameporwa viwanja vyao akishirikiana na bwana ardhi anayeitwa Tony.

Tony ameuzia watu viwanja mara mbilimbili ameacha watu wamekufa kwa presha wala sio utani.Maeneo ya kichangani,masiwani na airport imetembea rushwa na viwanja wamepewa wenye nacho.Ummy yote haya unayajua. Achilia mbali aina yetu ile ya rushwa ya watu wanaopendana na nafasi za uongozi. Tanga hilo sio geni na wewe unajua Takukuru wanajua maamuzi hakuna. Umekua ukiogopa ili uchaguzi upite asije akakuengua. Sasa muengue maana nimwizi na hakuna asiyejua tanga hapo.Tena wanatumia nguvu fulani za ziada kuzima mambo.

Kupitia uzi huu jamii inatakiwa ijue kwamba nyumba yako imeoza,tandabui kibao, inanuka mafunyo na mainzi kibao,ifagie nyumba yako ndio uende kwa jirani vinginevyo hata hao ulio wasimamisha kazi warudishe.
 
Back
Top Bottom