Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Waziri Ummy amesema hakuna mgonjwa aliyelazwa huku wote wameruhusiwa kurudi nyumbani na wanaendelea na shughuli zao. Hii inaendana na sayansi inayojulikana kwa ugonjwa huu kuwa, ugonjwa huu unatibika kwa kutumia dawa ambazo zinapatikana katika vituo vya kutolea huduma za afya kote nchini.
Amesema timu ya ufuatiliaji imebaini kuwa, miongoni mwa watu waliotangamana na wagonjwa hao (contacts) hakuna aliyeonyesha dalili za ugonjwa huu hadi kufikia sasa. Hii inadhihirisha pia, ni mara chache ugonjwa huu huambikizwa kutoka binadamu mmoja kwenda kwa mwingine.
Vilevile, wataalamu wanaendelea na utafiti wa kina kwa binadamu, wanyama na mazingira yanayowazunguka ili kubaini na kuweka mikakati ya kuudhibiti ugonjwa huu nchini.