Umoja wa Afrika (AU) yataka mazungumzo badala ya nguvu za kijeshi Venezuela

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Umoja wa Afrika (AU) umeeleza kuwa una “wasiwasi mkubwa” kufuatia mashambulizi ya kijeshi ya Marekani dhidi ya Venezuela na hatua ya kukamatwa kwa Rais Nicolás Maduro na utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump.

Katika taarifa iliyotolewa Jumamosi, AU ilisisitiza kuwa inaendelea kushikilia kwa dhati misingi ya sheria za kimataifa, ikiwemo heshima kwa uhuru wa nchi, mipaka yake ya kieneo na haki ya watu kujitawala, kama ilivyoainishwa katika Mkataba wa Umoja wa Mataifa (UN).

“Umoja wa Afrika unathibitisha tena dhamira yake thabiti ya kulinda kanuni za msingi za sheria za kimataifa, ikiwemo kuheshimu uhuru wa mataifa, mamlaka yao ya kieneo na haki ya watu kujiamulia mustakabali wao,” ilisema AU katika taarifa hiyo.

AU ilionya kuwa matumizi ya nguvu za kijeshi bila ridhaa ya nchi husika yanahatarisha amani ya kimataifa na kudhoofisha mfumo wa utawala wa dunia.
​

Mashambulizi ya Marekani dhidi ya taifa hilo tajiri kwa mafuta yameibua hasira na kulaaniwa kimataifa, huku yakizua maswali makubwa kuhusu mwelekeo na uhalali wa mfumo wa sasa wa utawala wa dunia.

AU ilisisitiza umuhimu wa mazungumzo, utatuzi wa migogoro kwa njia ya amani na kuheshimu mifumo ya kikatiba na taasisi za nchi, katika roho ya ujirani mwema, ushirikiano na kuishi kwa amani kati ya mataifa.

Umoja wa Afrika ulisisitiza kuwa changamoto tata za ndani zinazoikabili Venezuela zinaweza kushughulikiwa kwa njia endelevu tu kupitia mazungumzo ya kisiasa jumuishi miongoni mwa Wavenezuela wenyewe, bila shinikizo au uingiliaji wa nje.

Aidha, AU ilieleza mshikamano wake na wananchi wa Venezuela na kutoa wito kwa pande zote husika kujizuia, kuwajibika na kuheshimu sheria za kimataifa ili kuzuia kuzorota kwa hali ya usalama na kulinda amani na utulivu wa kikanda.

Wakati huo huo, serikali ya Afrika Kusini imetoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuitisha kikao cha dharura kujadili mashambulizi ya kijeshi ya Marekani dhidi ya Venezuela na kukamatwa kwa Rais Maduro pamoja na mkewe.

Katika taarifa yake ya Jumamosi, Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini ilisema matumizi ya nguvu za kijeshi bila uhalali wa kimataifa yanadhoofisha uthabiti wa mfumo wa kimataifa na kanuni ya usawa kati ya mataifa.
​
 
Hao A.U Hawakuona yaliyotokea tz?

Kwa nini wasingetuma jeshi
 
This organization is completely irrelevant. Wamewahi kumuondoa dictator gani kwa mazungumzo? The continent continues to be home to some of the most evil dictators!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…