Umoja wa Machifu mkoa wa Mara watoa ONYO kwa wanasiasa wanaotoa matamshi ya kutotambua umuhimu wa Machifu nchini

Hawatafanikiwa kutugawa....wanapoteza muda tu.
Mimi issue za mila na uchifu sina hamu nazo maana zitaongeza uchawi na ushirikina kwenye jamii! Ndugu wengi sana wameuawa kwa uchawi na kama unaangalia hivi sasa nchi mauaji kila kona chanzo ni mambo haya ya kijinga ya kukabidhi nchi kwa machifu!
 
Kati ya vitu vya kijinga na kipumbafu alivyovishabikia Rais Samia ni hili suala la Machifu. huu ni ujinga mkubwa.

Raisi samia kama anaupenda uchifu wa bara basi aende zanzibar aurudhishe usultani.

kurudisha uchifu ni sawa na kuongeza ukabila, udini, nk
 
Sio tu ni sawa na... Bali nikuongeza mgawanyiko tulokwisha kuusahau.
 
Zama hizi machifu....!? Wa huku kwetu wanatumika wakati wa uchaguzi ukipita hawana ishu maana hata wanaotambika wamepungua sana
 
Pamoja na kupewa heshima kubwa, watu wanawapelekea vitu kama kuku,kondoo, ng'ombe,mbuzi,magunia ya mpunga,mahindi,mtama, nk. Unadhani wataachaje kutetea kwa nguvu kubwa ulaji wao huo?
 
hakika njaa mbaya sana mtu mzima unaweza kujivunjia heshima kisa njaaaaaaaaaa
 
naona na tishirt wametengemezewa
 
Sasa chifu hangaya ni chifu wa kisukuma sio chifu wa mara wao wanamtambua vipi kama chifu wao.

Walisema ili swala la machifu linaanza mdogo mdogo litakua kubwa na limeaanza
Ukomo wa hili sual la machifu ni kutumbukia kwenye shimo la ukabila.
Make uchifu upo ndani ya kabila au koo.
Tushaanza kuwachanganya vijana wetu! Kinachoendelea si sahihi Katika taifa linalopinga ukabila alafu linakumbatia uchifu
 
Suala la kuukuza uchifu TZ linaturudisha nyuma.Hayati J.K. Nyerere aliona mbali.Kama serikali ya ccm inaona halina madhara basi himizeni kila kabila lifufue uongozi wa kichifu.
Ni ujinga mtupu wanatafuta posho za kuitwa kwenye sherehe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…