mabutu1835
JF-Expert Member
- Nov 25, 2018
- 909
- 1,425
Ni miaka zaidi ya 60 tangu tupate uhuru na hata kufikia muungano na kutengeneza taifa linaitwa Tanzania. Punde baada ya uhuru Mwl. J.K.Nyerere alitangaza maadui wa maendeleo; Ujinga, Umaskini na Maradhi. Mikakati mbalimbali ilibuniwa na kutekelezwa kupambana na maadui hao hadi leo.
Ila inasikitisha na kuhuzunisha uanzishwaji na uendeshaji wa umoja wa makabila unaofanya na wanafunzi wa elimu ya juu katika vyuo mbalimbali, mf; Umoja wa wakinga, Umoja wa Warangi,Umoja wa wahaya, Umoja wa wachaga, nk
Ni ushamba na ufinyu wa fikra unaodhihirishwa na wasomi wetu.Ningetegemea waanzishe umoja na makundi mengine ya wataalamu ili kukuza taaluma au ujuzi katika viwango vya juu kwa manufaa ya Taifa.
Muendelezo wa ukabila kwa namna yoyote katika vyuo vya elimu ya juu ni ufinyu wa fikra na uthibitisho wa umaskini wa fikra wa wasomi wetu.
Badilikeni vijana na wasomi wetu, tupinge ukabila na hata udini kwani ni adui wa maendeleo katika taifa lolote.