Umoja wa Mataifa kupunguza mgao wa chakula na fedha kwa wakimbizi

Umoja wa Mataifa kupunguza mgao wa chakula na fedha kwa wakimbizi

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa limesema zaidi ya wakimbizi milioni 1.2 nchini Uganda watapunguziwa mgao wa fedha na chakula kuanzia mwezi Februari kutoka kwa wafadhili wa kimataifa.

Shirika hilo la WFP ambalo limeshinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka huu, limepokea nusu tu ya fedha inazohitaji ili kuhudumia wakimbizi nchini Uganda.

Msemaji wa WFP, Tomson Phiri, ameuambia mkutano wa waandishi habari kuwa mgao uliopunguzwa utakidhi asilimia 60 ya mahitaji ya wakimbizi hao.

Nchi hiyo ya Ukanda wa Afrika Mashariki, ni miongoni mwa nchi barani Afrika zenye idadi kubwa ya wakimbizi. Uganda inahifadhi wakimbizi ambao wamekimbia mapigano nchini Congo, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan Kusini na Burundi.
 
Back
Top Bottom