beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Maafisa wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, wameitaka Uganda kudhibiti vurugu za vikosi vya usalama na kuwaondolea mashitaka wapinzani wa kisiasa na wanaharakati waliokamatwa katika kile walichokitaja kuwa ni ukandamizaji wa uchaguzi.
Katika taarifa yake, wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamesema wana wasiwasi mkubwa na vurugu zinazohusiana na uchaguzi, matumizi ya nguvu kupita kiasi ya vikosi vya usalama pamoja na ongezeko la ukandamizaji dhidi ya maandamano ya amani.
Mwanamuziki Bobi Wine ambaye jina lake ni Robert Kyagulanyi ameonekana kuwa mpinzani mkubwa wa Rais Yoweri Museveni katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa rais utakaofanyika Januari 14.
Katika kipindi cha miezi mitano iliyopita, kumekuwa na mashambulizi 16 dhidi ya waandishi wa habari wanaofuatilia ripoti za uchaguzi