Juni 7, 2023, Mtumiaji Mmoja wa Mtandao wa Twita aliweka chapisho linaloonesha kuwa Umoja wa Mataifa umeruhusu watu kushiriki Mapenzi na watoto.
Andiko hilo limezua sintofahamu kubwa kwenye mtandao huo kwa taasisi yenye nguvu kubwa duniani kutoa tamko la aina hiyo.
Tunaomba kufahamu ukweli wake.
Andiko hilo limezua sintofahamu kubwa kwenye mtandao huo kwa taasisi yenye nguvu kubwa duniani kutoa tamko la aina hiyo.
Tunaomba kufahamu ukweli wake.
- Tunachokijua
- Andiko lenye lugha ya kiingereza linalosomeka kama “Pedophilia is not a crime” lilianza kusambaa kwenye mtandao wa Twita mnamo Juni 7, 2023.
Andiko hili lenye maana ya “Kutamani watoto Kingono (Kimapenzi) sio uhalifu” linadaiwa kutolewa kwenye kurasa rasmi za Umoja wa Mataifa.
Ukweli wake upoje?
Andiko hili halina ukweli wowote. JamiiForums haijapata ushahidi kutoka kwenye kurasa Rasmi za Umoja wa Mataifa.
Pia, JamiiForums haikupata taarifa zozote za Makavazi ya andiko hili kama limefutwa kwa kutumia kanzi data za PolitiTweets kutoka kwenye taasisi Maarufu Duniani, ikiwemo Umoja wa Mataifa.
Sehemu nyingine ya ushahidi unaoweza kutumika kuthibitisha uzushi huu ni kutumia alama za uthibitisho wa Akaunti za Twita zinazotolewa na Kampuni hiyo ambao akaunti halisi ya Umoja wa Mataifa huwa na uthibitisho wa alama ya Kijivu (Gray).
Kwa mujibu wa Sera za Mtandao wa Twita, Rangi hii humaanisha akaunti husika anamaanisha kuwa Serikali au Taasisi kubwa ya Kimataifa. Hata hivyo, akaunti inayosambaza uzushi huu imewekewa alama ya uthibitisho yenye rangi ya bluu (Blue).
JamiiForums imebaini pia kuwa Picha hiyo inayosambaa ilitengenezwa na mhusika ambaye malengo yake ya kufanya hivyo hayajajulikana kwa kuwa siku hiyo hakukuwa na chapisho lolote la Umoja wa Mataifa linaloweza kuhaririwa baadhi ya taarifa zake.
Hadi kufikia Juni 12, 2023, Saa 3:00 asubuhi, Andiko hili lilikuwa limesomwa na zaidi ya watu 112,300, ilipendwa mara 3,811 na ilishirikishwa mara 173.