Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Nchi za Umoja wa Ulaya zimekubaliana kurahisisha safari za watalii waliochanjwa dhidi ya Covid-19 au waliougua na kupona ugonjwa huo.
Baraza la umoja huo wenye wanachama 27 limependekeza kuwa kuanzia mwezi ujao, masharti ya karantini yaondolewe kwa watu wanaowasili katika nchi hizo wakiwa wamepokea chanjo iliyoidhinishwa na Umoja wa Ulaya pamoja na shirika la Afya Ulimwenguni, WHO.
Halmashauri ya Umoja wa Ulaya ambayo ndiyo yenye majukumu ya kiutendaji imekaribisha pendekezo hilo lisilo la kisheria, ambalo pia limetaka watoto wasio na umri wa zaidi ya miaka 6 wasilazimike kupimwa pale wanaposafiri na watu wazima.
Chanjo zinazotambuliwa na Umoja wa Ulaya ni zile zilizotengenezwa katika nchi za magharibi ambazo ni Pfozer-BioNTech, Moderna, AstraZeneca, Johnson&Johnson na Novavax.