Umoja wa Ulaya umekubali kuiongezea Uingereza muda wa kujiondoa katika umoja huo

Umoja wa Ulaya umekubali kuiongezea Uingereza muda wa kujiondoa katika umoja huo

The Assassin

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
4,942
Reaction score
20,077
Mpango wa Uingereza kujiondoa umoja wa Ulaya tarehe 31.10.2019 kama alivyoapa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza, Borris Johnson umeshindikana hivyo wameomba muda zaidi kwa Umoja wa Ulaya ili waweze kujiandaa zaidi na kupata makubaliano mapya yatakayokubaliwa na Bunge la Uingereza.

Borris aliapa kuwa iwe mvua iwe jua, iwe mchana iwe usiku tarehe 31.10.2019 ilikua lazima Uingereza ijiondoe EU ila mipango yake imegonga mwamba, Wabunge waliungana kuhakikisha huo mpango wa ghafla na usio na maslahi mazuri kwa Waingereza unakwama

Tusisahau Uingereza ndio nyumbani kwa demokrasia, Kiongozi hajiamulii tu kila anachowaza kama huku kwetu. Waingereza wanatufundisha kuwa inapokuja maslahi ya nchi chama hakina nafasi.

==================

European leaders have agreed to the UK's request for a three-month Brexit extension, the EU Council President Donald Tusk has tweeted.

He said the "flextension," which can be shortened if Britain passes a deal in the meantime, is set to be formalized soon.

This is the delay that Johnson insisted he would never request -- but his hands were tied when Parliament forced an extension if the Prime Minister couldn't pass his exit deal.

The news could now swing opposition MPs towards supporting Johnson's attempt to force a snap general election later.


Source: CNN
 
Safi kabisa huku mtu akitoka bafuni tu na taulo lake mawazo aliyopata huko bafuni/chooni anayaleta kwa wananchi.

Hovyo kabisa...!
 
Tatzo huku kwetu hata wabunge wenyew hawana msimamo

wapo kwa ajil ya maslah yao na sio maslai ya nchi yao na ndio maana wanakosa nguvu na support ya kutosha kutoka kwa wanachi ambao walimuweka madarakan
 
Tusisahau kwamba mpango kama huu uliwahi kuwasilishwa na Theresa May kwa karibu Mara mbili katika kipindi chake cha uongozi wa Uingereza, na huu ulikuwa mpango wake uliolenga Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya.
Pamoja na kwamba tunakumbuka jinsi Theresa May alivyo kuwa mwenye nguvu, lakini alijikuta anaishia kugonga mwambabaada ya kupingwa na wabunge kwa mara ya pili huku zikiwa zimesalia siku 17 hadi muda wa taifa hilo kujitoa katika EU.
 
DEMOKRASIA..ipi..ndo kusema na sie tuwe na Ufalme..maana nachoona UK.. Tarishi ndo analalamikiwa na wananchi.
 
Back
Top Bottom