Strong ladg
Senior Member
- Jul 15, 2021
- 170
- 445
Niamey , Brussels.
Umoja wa Ulaya( EU) umemuita nyumbani balozi wa Umoja huo nchini Niger leo tarehe 23 Novemba 2024. Hatua hiyo imekuja baada ya serikali ya Niger kuukosoa umoja huo kwa kitendo cha kupeleka msaada nchini Niger bila kuipa taarifa serikali ya Niger.
Katika tarifa yake serikali ya Niger imesema kuwa kitendo cha Umoja wa Ulaya kupeleka msaada kwa ajili ya waathirika wa mafuriko yalitokea nchini humo miezi michache iliyopita na kuifikisha moja kwa moja kwenye shirika la msalaba mwekundu na shirika la kuhudumia wakimbizi la Denmark bila kuitaarifu serikali ni kuingilia uhuru wa nchi. Serikali pia imeagiza kufanyike ukaguzi Ili kujiridhisha kama kweli fedha hizo za msaada zilitumika kama ilivyopaswa au zilipelekwa kwenye shughuli nyingine zinazoweza kuhatarisha usalama wa nchi.
Itakumbukwa kuwa mwaka uliopita uhusiano kati ya Niger na Umoja wa Ulaya uliathirika baada ya Umoja huo kutangaza kutoitambua serikali ya kijeshi iliyoingia madarakani baada ya kumpindua aliyekuwa Rais kibaraka wa Ufaransa Mohamed Bazoum. Umoja wa Ulaya ulikwenda mbali zaidi hata kufikia hatua ya kuiwekea vikwazo Niger ambapo Niger ilijibu kwa kuvunja mikataba ya kijeshi na ile ya kudhibiti idadi ya wahamiaji wanaopita Niger kuelekea Ulaya iliyokuwa imesainiwa kati ya Niger na EU
Vyanzo: Tovuti ya EU, Shirika la habari la Niger ( RTN). Sahel Info TV