Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya leo imepitisha sheria ambazo zitafanya cheti cha covid-19 cha Umoja huo kuwa halali kwa usafiri miezi tisa baada ya kukamilika kwa ratiba ya kimsingi ya chanjo. Haya ni kwa mujibu wa afisa mmoja wa Umoja huo. Sheria hizo mpya zitaanza kutumika katika mataifa 27 wanachama wa Umoja huo kuanzia Februari 1.
Sheria hizo zinaweza kupingwa na wingi wa mataifa katika Umoja huo ama wingi wa wabunge katika bunge la Ulaya lakini maafisa wanasema kuna uungwaji mkono wa kutosha.
Baada ya sheria hizo kuanza kutumika, mataifa ya Umoja wa Ulaya yatalazimika kuruhusu wasafiri waliopata chanjo kamili na cheti halali kuingia katika maeneo yao.
Hata hivyo kulingana na hali kuzidi kuwa mbaya, mataifa hayo yanaweza kuweka vizuizi zaidi kama vile kuthibitishwa kutokuwa na maabukizo ama karantini.